Watoto wachanga wafariki Kwa moto hospitalini
Takriban watoto sita waliozaliwa wamefariki kufuatia moto katika hospitali moja huko Delhi, kulingana na polisi.
Moto huo ulizuka Jumamosi Mei 26,2024 jioni katika hospitali moja eneo la Vivek Vihar katika mji mkuu wa India.
Kulikuwa na watoto 12 katika kitengo hicho, afisa mkuu wa polisi Surendra Choudhary alisema. Mwingine alifariki kabla ya moto kuanza.
Mamlaka ilisema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki wa hospitali hiyo aliyetoroka.
Picha za kusikitisha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha milipuko kadhaa ya moto ukiwa umeteketeza jengo zima.
Waziri Mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal alisema moto huo "unahuzunisha moyo".
"Sababu za tukio hilo zinachunguzwa na yeyote atakayehusika na uzembe huu hataachwa nje," Bw Kejriwal alisema.
Mkurugenzi wa idara ya zima moto mjini Delhi Atul Garg ameliambia shirika la habari la Press Trust of India kwamba lori 14 za zimamoto zilitumwa kukabiliana na moto huo.
"Moto ulisambaa kwa kasi sana kutokana na mlipuko wa mtungi wa oksijeni," alisema
0 Comments:
Post a Comment