SHULE YA SEKONDARI MADIVENI YAJENGEWA VYOO VYA KISASA
Na Gift Mongi, SAME
WANAFUNZI 215 shule ya Sekondari Madiveni iliyopo kata ya Msindo wilayani Same wameondokana na adha ya kukumbwa na maradhi mbalimbali ambayo wangeweza kuyapata hapo awali kufuatia vyoo walivyokuwa wanatumia kukosa ubora unaotakiwa.
Shirika la Mater Dei Africa limekamilisha ujenzi wa mradi wa vyoo viwili vyenye jumla ya matundu 10 pamoja na Tanki la kuhifadhia maji ujazo wa lita elfu therasini ambapo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 32 kati yake takribani Shilingi milioni 1.5 nguvu kazi za wananchi.
Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amewashukuru Mater Dei kwa kusaidia Serikali katika kuhakikisha huduma zote muhimu ambazo wananchi wanatakiwa kuzipata kutoka kwa Serikali zinawafikia kwa wakati.
"Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inathamini sana mchango wa sekta binafsi ikiwemo kwenye ujenzi wa maendeleo, niwashukuru sana wadau wetu na niwaombe muendelee na sehemu nyingine ambazo bado zinauhitaji ndani ya wilaya yetu ya Same". Alisema Kasilda.
Awali akiwasilisha taarifa utekelezaji wa mradi huo, Julius Tarimo Meneja miradi mater Dei Africa amesema ujenzi huo ni sehemu ya uboreshaji wa Miundombinu ya shule lakini pia kwa wanafunzi ambao hapo awali walikuwa hatarini kupatwa magonjwa mbalimbali
0 Comments:
Post a Comment