MBUNGE AJA NA WAZO MBADALA KWA WAFUGAJI. ATAKA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUWAKOPESHA MBEGU BORA ZA MITAMBA KWA WAFUGAJI... BAADA YA HAPO SERIKALI IWADAI MAZIWA NA NYAMA..

 MBUNGE AJA NA WAZO MBADALA KWA WAFUGAJI.


ATAKA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUWAKOPESHA MBEGU BORA ZA MITAMBA KWA WAFUGAJI...


BAADA YA HAPO SERIKALI IWADAI MAZIWA NA NYAMA..


Na Gift Mongi, Dodoma


Katika kuhakikisha sekta ya mifugo nchini inakuwa na tija kwa wafugaji imebainika ni lazima kufuga kisasa ili kuweza kuendana na hali yaa soko inavyohitajika.


Kufuga kisasa inamaanisha kubwa mfugaji ataweza kunufaika moja kwa moja na kuweza kujikwamua kiuchumi tofauti na ilivyo hivi sasa.




Kwa maana hiyo basi mbunge wa  wa jimbo la Moshi Vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi(CCM) amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro umebarikiwa kuwa na ardhi nzuri kwa ajili ya ufugaji na kuiomba wizara ya Mifugo kuwekeza mbegu Bora (mitamba) ya Ng'ombe na wao wadai nyama na maziwa kutoka kwa wananchi. 


Prof. Ndakidemi alitoa kauli hiyo wakati akichangia makadirio ya  bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2024/2025.



0 Comments:

Post a Comment