Waziri Bashe Azitaka Taasisi za Kilimo Kuwekeza Zaidi katika Teknolojia

 

Dodoma, Aprili 30, 2024 – Waziri wa Kilimo,  Husein Bashe, amewahimiza taasisi na kampuni binafsi zinazohusika na kilimo kuongeza juhudi katika ubunifu na matumizi ya teknolojia ili kuongeza ufanisi na tija katika sekta hiyo.



Wito huo umetolewa leo wakati wa ziara ya Waziri Bashe katika maonesho ya kilimo yanayoendelea kwa siku tano katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Akiongea katika maonesho hayo chini ya kauli mbiu ya "From Lab to Farm," Waziri Bashe alisisitiza umuhimu wa teknolojia na ubunifu katika kuleta maendeleo ya kilimo.


Wakati wa ziara hiyo, Waziri Bashe aliweza kujionea mwenyewe mchango wa teknolojia na ubunifu katika kuboresha sekta ya kilimo. Hatua hii inalenga kuleta mapinduzi ya kisasa katika kilimo nchini kwa kufanya matumizi sahihi ya teknolojia katika shughuli za kilimo.


Kupitia kauli mbiu ya "From Lab to Farm," maonesho hayo yamekuwa jukwaa la kipekee kwa wadau wa kilimo kubadilishana mawazo, uzoefu, na kuonyesha mafanikio yao katika matumizi ya teknolojia katika kilimo.


Hivyo, wito wa Waziri Bashe unalenga kuhamasisha ushirikiano na uwekezaji katika teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha kuwa kilimo nchini kinakuwa cha kisasa, chenye tija, na cha kustawi zaidi.




0 Comments:

Post a Comment