Wasichana Waliookolewa Kutoka Boko Haram Wagoma Kurudi Kwa Familia Zao, Wafunga Ndoa na Waasi Waliowateka

 



Miaka kumi baada ya watu wenye silaha wa Boko Haram kumteka nyara binti yake kutoka shuleni katika mji wa Chibok nchini Nigeria, Yama Bullum anahisi kana kwamba amempoteza kwa mara nyingine tena.


Binti yake, Jinkai Yama, alikuwa mmoja wa wasichana 276 waliotekwa nyara kutoka shule ya upili mapema tarehe 14 Aprili 2014 na wapiganaji wa Kiislamu.


Hamsini na saba kati yao walitoroka muda mfupi baadaye. Kisha kati ya 2016 na 2018 wengine 108 waliokolewa na jeshi au kuachiliwa kupitia mazungumzo.


Wengine 91 bado hawajulikani walipo, lakini Bi Yama ni mmoja wa "wasichana 20 wa Chibok" waliookolewa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutoka kwa maficho ya Boko Haram katika Msitu wa Sambisa kaskazini-mashariki mwa jimbo la Borno, kitovu cha uasi wa miaka 15.


Lakini babake amekasirishwa na kugundua kuwa kama baadhi ya wanawake wengine walioachiliwa hivi majuzi, ameamua kubaki kuolewa na mmoja wa wapiganaji ambao aliwahi kumteka.


Wanandoa hawa sasa wanaishi katika mji wa Maiduguri - mji mkuu wa Borno, 125km (maili 78) kaskazini mwa mji wa mbali wa Chibok - katika makazi yaliyoandaliwa na gavana wa jimbo hilo Babagana Umaru Zulum.


"Sijafurahishwa na alichofanya gavana. Wasichana walifanikiwa kutoka msituni na gavana aliwaoza tena. Mamake amekasirika sana," Bw Bullum alisema.


Aligundua wakati binti yake alipompigia simu kumwambia Agosti mwaka jana - na akampa simu akimtaka azungumze na mumewe, muasi wa zamani.


Kufikia wakati huo, Bw Bullum alidhani kwamba alikuwa na mateka wengine walioachiliwa wa Chibok na watoto wake watatu katika mpango maalum wa ustawi.


Kama wazazi wengine kadhaa wa Chibok, Bw Bullum amesikitishwa na kile kinachoonekana kuwa kibali cha serikali ya Nigeria kuruhusu ndoa kati ya binti zao waliookolewa na wanaume waliowateka nyara.


Kuruhusu wanawake walioachiliwa kuishi na watekaji wao wa zamani kama wake.


Chanzo:BBC

0 Comments:

Post a Comment