Wanawake Jitokezeni katika Uongozi Simameni Imara kwenye Ushiriki na Utekelezaji

 



Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Arusha, Blandina Nkini, ametoa wito wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na majukumu ya uongozi.


Aidha amesisitiza umuhimu wa uwakilishi wa wanawake katika maamuzi na utekelezaji wa majukumu yao  kwani ushiriki wao ni muhimu sana katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii



Nkini ameyasema hayo leo wakati akifungua kongamano la wanawake wa jamii ya wafugaji, Wakulima na Waokota matunda linalofanyika jijini Arusha kwa siku mbili.


Amesema wanawake wanapaswa kuchukua nafasi zao katika uongozi siyo tu kwa kuchaguliwa, bali pia kwa kushiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi. 



Nkini amesisitiza kwamba ili kupata suluhisho la changamoto za kijamii kama mabadiliko ya tabia nchi na ukatili wa kijinsia, sauti za wanawake lazima zisikilizwe na kuzingatiwa.


Pamoja na hayo, Nkini aliomba jamii kuachana na mila na desturi zinazokandamiza wanawake na badala yake kukuza mila na desturi zinazosaidia katika maendeleo yao.

Alitilia mkazo haja ya kila mmoja kuchukua hatua katika kuhakikisha kwamba wanawake wanapata fursa sawa na wanaweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa jamii endelevu na yenye haki.




Naye Nailejileji Tipap kutoka Idara ya Jinsia  kutoka na PINGOs,  Forum amesisitiza umuhimu wa haki ya wanawake kugombea nafasi za uongozi uongozi wa umma bila woga na kutekeleza majukumu yao kwa dhati huku wakitetea haki za wananchi, hasa za wanawake, katika kutekeleza majukumu yao kwa jamii.






Kwa upande wake, Mratibu wa Masuala ya Haki za Wanawake PWC, Nalemuta Moisan anaelezea namna taasisi yao inavyoshiriki katika kuhakioisha wanawake wanapata haki ya kuthaminiwa na kuondoa ubaguzi wa kijinsia kwenye jamii ambapo pia hiwashirikisha wanaume kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji wa mikakati hiyo.



Neema Michael kutoka taasisi ya Ujamaa Community Resource Team, (UCRT) anasisitiza umuhimu wa wanawake kujitokeza kushiriki kwenye mikutano mikuu ya maamuzi na watoe michango yao ya mawazo yatakayosaidia kuleta usawa kwenye jamii ya wafugaji.



0 Comments:

Post a Comment