Serikali Yaongeza Bajeti ya Umwagiliaji Kwa Kukuza Sekta ya Kilimo

 

Dodoma, Aprili 30, 2024 – Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeongeza bajeti ya sekta ya umwagiliaji kwa lengo la kuimarisha sekta ya kilimo nchini. 



Bajeti hiyo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 46.5 mwaka 2021/22 hadi kufikia shilingi bilioni 373.5 kwa mwaka 2023/2024 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umwagiliaji.



Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema hayo wakati wa hafla ya kusaini mikataba ya miradi 20 ya umwagiliaji iliyofanyika leo mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majiliwa. 



Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Bashe alimshukuru Rais Samia kwa utashi wake wa kuwekeza katika miradi ya kilimo, hususani katika eneo la umwagiliaji.



Akifafanua zaidi, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, alieleza kuwa miradi hiyo itakapokamilika, itaongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 983,465.46, ambayo ni asilimia 81.9 ya lengo la kufikisha hekta 1,200,000 ifikapo 2025. 



Ongezeko hilo linatarajiwa pia kutoa ajira za kudumu kwa takribani watu 1,352,127.


Hatua hii inaonyesha dhamira ya serikali katika kukuza sekta ya kilimo kwa kuzingatia miundombinu imara ya umwagiliaji, ambayo itasaidia kuongeza uzalishaji, kuifanya kilimo kuwa cha kibiashara zaidi, na kuongeza pato la wakulima wadogo, hivyo kuboresha maisha yao.




0 Comments:

Post a Comment