SAMIA MGENI RASMI MEI MOSI ARUSHA

 

RAIS Samia suluhu Hasani anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani ,Mei Mosi yanayotarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Arusha.



Akiongea na vyombo vya habari Mkoani hapa, Rais wa Shirikisho la wafanyakazi Tanzania,TUCTA, Tumaini Nyamhokya alisema maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja wa mpira wa Sheikhe Amri Abeid siku ya Mei Mosi.


Alisema kauli mbiu ya mwaka huu inayosema,"Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha" inaakisi uhalisia wa Maisha ya wafanyakazi kwa sasa kwani gharama za maisha zimepanda na mishahara haikidhi Mahitaji ya kila siku ya Mfanyakazi.




Alisema mishahara ikiwa bora itawezesha mafao kuwa bora pia wakati wa kushtaafu .


"Hivyo basi tumeona ni Vema kutumia siku yetu hii muhimu ya Sherehe za Wafanyakazi kuikumbusha serikali na waajiri wote umuhimu wa kuwa na Mishahara bora inayoendana na hali halisi ya maisha tukiwa Kazini na baada ya kustaafu"


Katika maadhimisho hayo kiu ya  wafanyakazi wote nchini ni kutaka  kusikia serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inawaboreshea maslahi yao ikiwemo nyongeza ya mishahara ili waishi maisha bora.


"Sherehe za maadhimisho ya Mei Mosi zimekuwa zikifanyika kila mwaka na mwaka huu  zinafanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid  tukikumbuka wafanyakazi wenzetu walioteswa na kuuawa  wakipigania haki na maslahi yao"

 



Alisema Sikukuu ya wafanyakazi duniani hutumika kama fursa ya kuwasilisha changamoto za mfanyakazi kwa mwajiri ili kupata ufumbuzi juu ya changamoto hizo.


Alisema kuwa maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu 2024 yanaratibiwa na vyama 13 vinavyounda shirikishi la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA)ambavyo ni CHODAWU,COTWU(T),CWT,DOWUTA,RAAWU,TALGWU,TAMICO,TASU,TEWUTA,TRAWU,TPAWU,TUGHE na TUICO.


Aidha alisema Maadhimisho hayo yataenda sanjari na Michezo mbalimbali ya Mei mosi itakayofunguluwa rasmi siku ya jumamosi Aprili 21 mwaka huu na waziri  wa kazi ,vijana na Ajira na watu wenye ulemavu ,Deogrqtius Ndejembi. 


0 Comments:

Post a Comment