Majaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) wako katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa ajili ya mafunzo ya uandishi wa hukumu.
Katika mkutano wao na Naibu Mkuu wa IJA, Goodluck Chuwa, majaji hao wamepata ufahamu kuhusu historia ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.
Chuwa amewashukuru Majaji hao pamoja na Sekretarieti yao kwa kuamua kuja kufanyia mafunzo yao Chuoni hapo akisema kuwa hiyo ni heshima na sifa adhimu kwa Chuo na Wilaya ya Lushoto.
Naibu Mkuu huyo amewaomba majaji hao kurudi tena kwa mafunzo mengine kwani chuo kina miundombinu bora na rasilimali za kutosha kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.
Kwa upande wake, Rais wa EACJ, Jaji, Nestor Kayobera, ameipongeza IJA kwa mazingira mazuri na amefurahishwa na ushirikiano uliopatikana.
EACJ ilianzishwa mwaka 2001 na inajukumu la kutafsiri sheria za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoa maoni na ushauri wa kisheria, pamoja na kufanya usuluhishi
0 Comments:
Post a Comment