Mafuriko Yasababisha Maafa Afrika Mashariki

Mafuriko Yasababisha Maafa  Afrika Mashariki 



Mafuriko makubwa yamesababisha mamia ya maelfu ya watu kuyahama makazi yao kote Afrika Mashariki  Mbapo  nchini Kenya waokoaji na mamlaka "wanajiandaa kwa uharibifu zaidi.



"Hali inaendelea kuwa mbaya. Kufikia jana usiku tulikuwa tukiripoti zaidi ya watu 70 walikufa kote nchini," Seneta Edwin Sifuna, Seneta wa Kaunti ya Nairobi iliyoathiriwa zaidi na mafuriko.


Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayohusishwa na hali ya hewa ya El Niño


 Sifuna aliongeza kuwa timu za uokoaji zinakadiria kuwa watu 100,000 wamelazimika kuyahama makazi yao.


Michael Aiyabei, mkuu wa kamati ya kitaifa ya kushughulikia majanga, pia ameelezea wasiwasi. "Tunajiandaa kwa wakati mgumu zaidi," alisema.


Zaidi ya watu 150 wamefariki kutokana na mafuriko katika nchi jirani ya Tanzania.


Nchini Burundi, karibu watu 100,000 wamekimbia makazi yao.

0 Comments:

Post a Comment