Histori Chanzo Mauaji ya Kimbari Rwanda ifundishwe kwa Watoto

Histori Chanzo Mauaji ya Kimbari Rwanda ifundishwe kwa Watoto



Wananchi wamejitokeza kwenye makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 30 ya kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda.



Akiongea kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa aa Arusha, Paul Makonda amesema vijana wanapaswa kujifunza kupitia matukio yaliyotendeka na kusababisha mauaji hayo ili kuhakikisha hayajirudii tena.


Naye Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Irene Isaka amesisitiza umuhimu wa wananchi na vijana wa EAC kujua historia ya mauaji hayo ili yasijirudie.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Diaspora wa Rwanda Ulimwenguni,  Murenzi Daniel amesisitiza umuhimu wa kukomesha viashiria vyote vya kibaguzi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.










0 Comments:

Post a Comment