'ROCK BLOCK' WAIANGUKIA SERIKALI

 'ROCK BLOCK' WAIANGUKIA SERIKALI

Na Gift Mongi,Rombo


Serikali imeombwa kuangalia namna ya kuwasaidia kifedha na wataalam kwa wazalishaji wa matofali yanayotokana na miamba lengo likiwa ni kuwezesha wananchi kuwa na makazi bora.


Matofali hayo ya miamba kwa miaka ya karibuni mkoani Kilimanjaro na maeneo jirani yameonekana kuwa kimbilio la wengi jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za ujenzi.


Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuzalisha matofali cha Rock Block Fabian Woisso amesema kuwa Kwa sasa kutokana na uhitaji huo mkubwa serikali ingewawezesha kimtaji itaweza kupunguza gharama za uendeshaji tofauti na sasa.



'Sisi kama Rock Block tuiombe serikali ione namna ya kutusaidia kimtaji lakini pia nyenzo halikadhalika na wataalam ili tuweze kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa zaidi ya hapa'anasema Woisso


Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo wa Rock Block ni kuwa mahitaji ya tofali hizo zitokanazo na miamba yanazidi kuongezeka kila siku kutokana na uiamara wake lakini pia gharama kuwa nafuu zaidi.



'Tofali kutoka Rock Block ni tofauti na zile ambazo zinatengenezwa na saruji kwani haziathiriwi na magadi au matatizo mengine kama zinavyoathiriwa nyingine'anasema


Anasema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni mtaji ambao kwa namna moja unaonekana kuathiri shughuli za uendeshaji ambapo pia unakwamisha baadhi ya mambo.



Woisso anasema tangu kuanza kwa uzalishaji huo mwaka 2014 hadi sasa kumeweza kupatikana kwa ajira za kudumu 35 na nyingine za muda na kama ungekuwepo mtaji angeweza kuongeza idadi ya wafanyakazi na pia uzalishaji.


Mhandisi wa kiwanda hicho Steve Malamsha anasema kuwa kuna uhaba mkubwa wa wataalam wa mitambo hivyo vyuo vya ufandi vijikite zaidi katika kuzalisha wataalam hao



Anasema kuwa hata wale ambao wanasoma ipo haja sasa kwenda kufanya kwa vitendo badala ya nadharia pekee jambo linalokosesha fursa nyingi za ajira hususan kwa wazawa.



0 Comments:

Post a Comment