KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPONGEZA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPONGEZA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

 
Na Mwandishi wetu- Dar es salaam
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yaridhishwa na juhudi zinazoendelea nchini za kuthibiti dawa za kulevya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  Dkt. Joseph Mhagama akizungumza na waraibu wanaopata matibabu katika Kliniki ya Methadone iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala  wakati wa ziara ya Kamati hiyo  Jijini Dar es salaam.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Joseph Mhagama wakati ilipotembelea Kliniki ya Methadone iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala pamoja na Ofisi za Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Jijini Dar es salaam.

Dkt. Mhagama alisema kuwa, kiwango cha dawa za kulevya kinachokamatwa kwa sasa ni mara nne ya kilichokuwa kikikamatwa awali hatua iliyotokana na kuongezeka kwa juhudi za ukamataji.

"Kuongezeka kwa idadi ya dawa za kulevya zinazokamatwa nchini haimaanishi kwamba uuzaji na uingizaji wa dawa hizi umeongezeka bali inamaanisha kuwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeongeza nguvu katika kuthibiti" Alisema Dkt. Mhagama.

Alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu)  Jenista Mhagama, pamoja na timu yake katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya hali ambayo inaonyesha dhahiri kuwa Watanzania wapo salama.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika kuhakikisha kuwa biashara za dawa za kulevya inadhibitiwa nchini,”Alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilipotembelea maabara ya  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya  Jijini Dar es salaam.


Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama alieleza kuwa, serikali inatambua tatizo linalowapata waraibu wa Dawa za kulevya ambapo Serikali imeweka programu ya dawati tiba mbadala wanayoipata warahibu na itaendelea kuongeza vituo vingi ili waraibu wengi wapate matibabu.

"Kwa sababu waraibu wakipona wakawa hawana shughuli za kufanya ni rahisi kurudi kule walipotoka hivyo kama Serikali tutajitahidi kuwapatia kazi mbadala ya kuwaingizia kipato," Alisema Mhagama.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikitembelea na kukagua Kliniki ya Methadone iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala  wakati wa ziara ya Kamati hiyo  Jijini Dar es salaam.


(HABARI PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)







Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo alibainisha kwamba waraibu kwa sasa wamepungua katika maeneo mbalimbali zikiwemo vituo vya usafiri na mitaani kutokana udhibiti wa dawa hizo kuongezeka.

0 Comments:

Post a Comment