NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Tanzania Bara

NEC yatangaza  Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Tanzania Bara


Dodoma, 15 Februari, 2023

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R) Jacobs Mwambegele (kushoto) akiongoza kikao cha Tume jijini Dodoma leo Februari 15,2024 ambapo pamoja na mambo mengine kilitangaza uchaguzi mdogo wa kata 23 za Tanzania Bara utakaofanyika Machi 20,2024. Kishoto kwake ni Katibu wa Tume na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Kailima R.K.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi,(NEC) leo imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 23 za Tanzania Bara. 

Kufuatia tangazo hilo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhani, ametaja ratiba ya uchaguzi huo kama ifuatavyo:


Tarehe ya Uchaguzi: 20 Machi, 2024Kutoa Fomu za Uteuzi: Kuanzia tarehe 27 Februari, 2024 hadi tarehe 04 Machi, 2024Uteuzi wa Wagombea: Tarehe 04 Machi, 2024Kampeni za Uchaguzi: Kuanzia tarehe 05 hadi 19 Machi, 2024


Uchaguzi huu umetangazwa kwa mujibu wa matakwa ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata 23 za Tanzania Bara, kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 13(1) cha sheria hiyo.


Kata zitakazofanya uchaguzi huo mdogo ni:


  • Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni)
  • Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji)
  • Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora)
  • Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha)
  • Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo)
  • Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti)Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga)
  • Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea)
  • Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe)
  • Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa)
  • Mshikamano (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma)
  • Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama)
  • Nkokwa (Halmashauri ya Wilaya ya Kyela)
  • Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba)
  • Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu)
  • Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema)
  • Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba)
  • Kabwe (Halmashauri ya Nkasi)Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu)
  • Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza)
  • Boma (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga)
  • Mtimbwani (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga)
  • Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga)


Tume inatoa wito kwa vyama vya siasa, wagombea, na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo, na maelekezo ya Tume katika kipindi cha uchaguzi huu mdogo.

0 Comments:

Post a Comment