MBUNGE AFANIKISHA UPATIKANAJI WA BARABARA

 MBUNGE AFANIKISHA UPATIKANAJI WA BARABARA


Na Gift Mongi-Moshi



Wakazi katika kata ya Kibosho Magharibi katika jimbo la Moshi Vijijini kwa sasa wanamatumaini ya kuwa na barabara yenye kupitika muda wote ambapo ujenzi wake kwa sasa unaendelea.



Barabara hiyo ni ile ya Weruweru - Manushi - Kombo yenye urefu wa kilomita 10.2 na ipo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024


 Mkazi wa eneo hilo Gerson Mallya anasema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kunaenda kuchochea maendeleo ambayo hapo awali hayakwepo 


'Ukishakuwa na barabara yenye kupitika kipindi chote cha mwaka ni uhakika kuwa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zitaenda kuongezeka'anasema


Kwa mujibu wa Gerson ni kuwa kupatikana kwa barabara hiyo  ni matokeo ya kilimo cha muda mrefu kutoka kwa wananchi hao ambapo diwani na mbunge waliweza  kusikiliza na kuona manufaa yake.


'Hapa ni lazima tumshukuru sana mbunge wetu Prof Patrick Ndakidemi na diwani kwa ujumla Kwa kuweza kusikiliza kilio chetu na sasa kama unavyoona kazi ina ndelea'anasema       


Damas Mushi anasema kuwa mbunge wao Prof Ndakidemi kwa kipindi kirefu amekuwa akipigania barabara na kuwa anaamini kuwa ni kichocheo kimojawapo katika maendeleo


Anasema mradi huu ukikamilika utaondoa adha kubwa ya usafiiri hususani wananchi wa vijiji vya Kombo, Manushi Ndoo,  Sinde na Kata za jirani.


Mkandarasi aliyepewa zabuni hiyo ni Brand Mark Contractor Ltd. Ambapo wanatagemea kukabidhi mradi huo kufikia tarehe 02/06/2024. 




0 Comments:

Post a Comment