15 WAFARIKI AJALI ILIYOHUSISHA LORI NA MAGARI MADOGO MATATU, SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYOMBO VYA USALAMA

 15 WAFARIKI  AJALI ILIYOHUSISHA LORI NA MAGARI MADOGO MATATU, SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYOMBO VYA USALAMA



Watu kumi na tano wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha lori na magari mengine madogo matatu katika eneo la by Pass Ngaramtoni wilaya Arumeru Mkoa wa Arusha.



Akitoa taarifa hiyo katika eneo la ajali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP, Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea februari 24,2024 muda wa saa 11 jioni ambapo iliyohusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la Ngaramtoni Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.


Kamanda Masejo amesema wanaendelea na uchunguzi wakina  kubaini chanzo haiisi cha ajali hiyo.


Aidha amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya mount Meru kutambua miili ya waliofariki katika ajali hiyo.


RAIS ATUMA SALAMU ZA POLE 

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya watu 15 katika ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, mkoani Arusha," anaandika Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ukurasa wake wa X Na kuongeza.


"Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliopoteza jamaa zao katika katika ajali hii. Ajali hizi zinachukuwa wapendwa wetu, nguvu kazi ya Taifa na mihimili ya familia. Naendelea kutoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria za usalama barabarani katika matumizi ya vyombo vya moto. 


"Naagiza vyombo vyetu vya ulinzi, usalama na udhibiti kuendelea kuhakikisha vinasimamia sheria kikamilifu, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri na udhibiti wa leseni kwa madereva wanaorudia kuvunja sheria mara nyingi na wakati mwingine kusababisha watu kupoteza maisha.


"Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina,".



0 Comments:

Post a Comment