KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MASHAMBA ,VIWANDA VYA SUKARI VYA MKULAZI NA MTIBWA

 KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MASHAMBA ,VIWANDA VYA SUKARI VYA MKULAZI NA MTIBWA


Na Gift Mongi,Morogoro

 Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi akiwa katika Mashamba ya miwa ya kiwanda cha Sukari cha Mtibwa pamoja na wanakamati wenzake na watumishi wa shamba la Mtibwa. 




Kamati ya kudumu ya bunge viwanda biashara kilimo na mifugo wametembelea mashamba ya  miwa ya Mkulazi (Wilaya ya Kilosa) na Mtimbwa (Wilaya ya Mvomero) na viwanda vyake vya sukari.


Miongoni mwa mjumbe katika kamati hiyo ni  mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ambaye pia alieleza dhumuni la ziara hiyo muhimu mjumbe wa kamati hiyo.


Kwa mujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa ziara hiyo ilikuwa mahsusi kufuatilia uzalishaji wa sukari kwenye viwanda hivyo katika kipindi hiki cha mvua za El Nino zinazoendelea nchini. 


Wajumbe wa kamati walijionea uharibifu mkubwa wa miundombinu uliosababishwa na mvua na kuzorotesha uzalishaji wa sukari. 


'Ziara hii ni muhimu kwetu tumejionea uharibifu uliofanyika lakini pia tumepata angalau wasaa kuweza kuishauri serikali'alisema

Prof Ndakidemi yuko na msemaji mkuu wa timu ya Mtibwa SUGAR, Tobias Kifaru







0 Comments:

Post a Comment