Rombo, Desemba 29, 2023 - Beatrice James Minja, mkazi wa Tarakea, Rombo, amelazwa hospitalini akipambana na maisha yake baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa visu 25 na Paul Tarimo, aliyedaiwa kuwa mfanyakazi wa Prof.Adolf Mkenda, Mbunge wa Rombo na Waziri wa Elimu.
Inaelezwa kuwa Beatrice na Paul walikuwa katika mahusiano yenye vurugu, ambapo Beatrice alikumbwa na unyanyasaji wa mara kwa mara, ikiwemo kipigo kilichosababisha kupoteza mimba. Baada ya juhudi za kutafuta suluhu kushindikana, Beatrice aliamua kuondoka na kuanza upya maisha yake.
Kabla ya kuondoka, Tarimo alimpora Beatrice kiasi cha 10M ambazo zilikuwa mtaji wa biashara na pesa za ujenzi wa nyumba ya mama yake. Beatrice aliripoti tukio hilo polisi, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Beatrice aliacha mali nyumbani, ikiwemo nguruwe sita na vitoto 11, lakini Tarimo alikata nguruwe wote na vitoto baada ya kuondoka. Polisi hawakuchukua hatua yoyote.
Novemba 12, 2023, Beatrice akiwa na wanawake wengine wawili alishambuliwa na Tarimo, ambaye alimchoma visu 25.
Beatrice alikimbizwa hospitali ya Huruma kisha kupewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo Moshi ambapo tayari amefanyiwa upasuaji mkubwa mara mbili wa tumbo na majeraha zaidi ya 20 yameshonwa.
Yupo kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku hali yake ikielezwa kuwa bado si nzuri.
Wakati huo huo, Tarimo anaendelea na shughuli zake kama kawaida, licha ya madai ya shambulizi hilo huku akidaiwa ametishia kuwasaka na kuwaua watoto wa Beatrice, ambao tayari wameripoti kutishiwa maisha kwenye kituo cha polisi Tarakea ingawa hakuna hatua zozote zimechukuliwa dhidi yake mpaka sasa.
Juhudi za kumpata Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa kuzungumzia suala hilo hazikuxaa matunda kwani simu yake ilikuwa ikiita muda wote bila kupokelewa.
Jamii inaendelea kuomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kuleta haki kwa Beatrice na kumlinda familia yake
0 Comments:
Post a Comment