WIKI YA AZAKI 2023 KUANGAZIA TEKNOLOJIA NA JAMII


Mkutano wa wiki ya AZAKI CSO Week 2023 unatarajiwa kuanza rasmi kesho jumatatu,Oktoba 23,2023 jijini Arusha, ukiwa na kauli mbiu "Tech and Society, Now and Beyond," ambayo inasisitiza uhusiano kati ya teknolojia na jamii na jinsi inavyoweza kuchangia maendeleo ya Tanzania.


Mwenyekiti wa kamati ya wiki hiyo, Nesia Mahenge amewaeleza waandishi wa habari kuwa ,kutano huo utawaleta pamoja wadau mbalimbali, wakiwemo asasi za kiraia, watunga sera, wataalamu wa teknolojia, na wadhamini wa maendeleo, kwa lengo la kujadili na kushirikishana mawazo kuhusu jinsi teknolojia inaweza kutumika kwa manufaa ya jamii.


Balozi wa Uswisi,  Didier Chasot anatarajiwa kutoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jambo linaloonyesha mahusiano mazuri yaliyopo baina ya AZAKI na wadau wa maendeleo katika kuimarisha sekta ya asasi za kiraia nchini Tanzania.

Mahenge amesema kuwa mengine yanayotarajiws kujadiliwa kwenye  mkutano huo ni pamoja na hotuba kuu ya ufunguzi inayoitwa "Tech and Society," itakayotolewa na Abuubakar Ally, mwakilishi kutoka kampuni ya teknolojia, Apple Inc. 

Majadiliano ya washiriki yanalenga kuchunguza jinsi teknolojia inavyobadilisha maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na afya, elimu, na kilimo, na jinsi inavyoweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

"Washiriki watajadili masuala kadhaa yanayohusiana na teknolojia na jamii, kama vile matumizi ya teknolojia katika elimu, mabadiliko ya kidigitali katika uchaguzi na demokrasia, ujasiriamali unaoongozwa na vijana katika enzi ya kidigitali, na maswala ya jinsia na teknolojia kwa lengo la kushughulikia pengo la kidijitali kati ya wanaume na wanawake," amesema Mahenge na kuongeza.

...Mkutano pia unaweka mkazo kwenye masuala ya kifedha na matumizi ya teknolojia kwa kuingiza wengi katika huduma za kifedha. Pamoja na hayo, utawala wa kidemokrasia na matumizi ya data wazi katika utawala yatajadiliwa kwa kina,".

"Kutakuwa na mjadala kuhusu maadili ya akili bandia (AI) na matumizi ya AI kwa faida ya kijamii. Pia, wadau watashughulikia masuala ya usalama wa mtandaoni na ulinzi wa data kwa Asasi za Kiraia (CSOs),".

Mahenge amesema kuwa mkutano huo utahusisha pia vikao vya kijamii vya kueneza teknolojia kwa maendeleo, ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji na zana za kidigitali za kilimo na upatikanaji wa masoko kwa wakulima wadogo.

Kauli mbiu ya "Tech and Society, Now and Beyond" inasisitiza jinsi teknolojia inaweza kuwa kichocheo cha maendeleo chanya ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania. Washiriki wanatarajiwa kubadilishana mawazo na kutoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kutumia teknolojia kwa faida ya wananchi wote na jinsi ya kupunguza pengo la kidijitali. CSO Week 2023 inaashiria jukwaa la kuelimisha na kubadilishana mawazo juu ya jinsi teknolojia inaweza kutumiwa kwa faida ya jamii na maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dr. Anna Henga amesema mijadala hiyo pia itajikita katika masuala ya kimaadili katika kupokea matumizi ya maarifa bandia (Artificial Intelectual) ili kuhakikisha kuwa maarifa hayo yanalenga kukabiliana na changamoto za kijamii na kuleta manufaa kwa jamii nchini Tanzania.


Naye Mwakilishi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Deogratius Temba amesema katika kuhakikisha kauli mbiu ya mwaka huu ya Teknolojia na Jamii inakuwa jumuishi kwa jamii yote, watahakikisha makundi yaishio pembezoni hususani wanawake nao wanafikiwa

0 Comments:

Post a Comment