NCAA WAKANUSHA KUUA MIFUGO YA WAFUGAJI NGORONGORO

SIKU tatu baada wa wananchi wa Ngorongoro kuibua madai mazito juu ya mifugo yao kufa baada ya kupewa madini ya chumvi yenye sumu na Mamlaka ya hifadhi ua Ngorongoro, (NCAA), taasisi hiyo imtoa taarifa kwa umma ikikana madai hayo.


Kanusho hilo limetolewa leo Oktoba 07,2023 na Afisa Uhifadhi Mwandamizi kitengo chw Uhusiano wa Umma wa taasisi hiyo, Kassim Nyaki limewaomba wananchi kupuuza taarifa hizo kwa madai kuwa si za kweli.

Kwenye taarifa hiyo kwa umma yenye kichwa cha habari  "kanusho kuhusu taarifa potofu za vifo vya mifugo ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro" imekiri kutoa chumvi ya mifugo kwenye vijiji vya Misigyo, Kayapus, Mokilal, Oloirobi na Irkepus tokea mwaka 2017.



Hata hivyo taarifa hiyo haikuzungumzia juu ya taarifa ya timu ya wataalam iliyoundwa na mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala kufuatilia suala hilo wala matokeo ya kimaabara yaliyotolewa baada ya kupima sampuli ya chumvi hiyo waliyoisambaza.

Awali wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kupitia mtandao wa Sauti Kubwa waliibua madai kuwa  madini ya chumvi yaliyosambaziwa na serikali 2021 iliua mifugo mingi ya wafugaji hivyo kuwafanya wananchi kuwa mafukara.

https://sautikubwa.org/chumvi-ya-serikali-yapukutisha-mifugo-ngorongoro/

Juhudi za kumpata mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa inaita muda wote bila kupokelewa hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu.

Kadhalika  juhudi za kumpata mkurugenzi wa kampuni ya vifaa vya ujenzi ya Panga, Marco Panga kupitia namba zake za simu mbili tofauti alizoweka kwenye nyaraka za kuingiza mzigo huo kutoka nchini Kenya hazikupatikana muda wote.

0 Comments:

Post a Comment