PAPA FRANCIS AMPA ASKOFU RUGAMBWA HADHI YA UKADINARI

 


Leo, tarehe 30 Septemba 2023, historia ya Kanisa Katoliki imeandikwa kwa alama za sherehe na utukufu huku Baba Mtakatifu Francis akimpa Hadhi ya Ukardinali Askofu Mkuu Protase Rugambwa, mwana wa Karagwe na mzaliwa wa Ukoo wa Abakaraza (Abarigi). Tukio hili kubwa limefanyika kwenye viwanja vya Mt. Petro, Vatican, ambapo jumla ya Maaskofu wakuu 21 wamepewa hadhi ya Ukardinali kutoka nchi mbalimbali duniani.


Kardinali Protase Rugambwa amejiunga na daraja hili kubwa la Ukardinali, akiwa ni Mtanzania wa tatu kufikia wadhifa huu wa heshima ndani ya Kanisa Katoliki, baada ya Baba Askofu Laurean Rugambwa na Mwadhama Polycarp Pengo. Majina yake ya kifamilia, "Protase Abakaraza," yamebeba historia ya heshima kwa Askofu Laurean Rugambwa, ambaye alimzuru Bukoba siku aliyozaliwa Protase.



Wakati wa sherehe hii kubwa, Kardinali Rugambwa ameonyesha mtamgamano wa Kanisa kwa kusindikizwa na viongozi mbalimbali wa Kanisa Katoliki na hata wawakilishi wa makanisa mengine. Miongoni mwa waliomtia moyo ni Askofu Dr. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, ambaye ameshuhudia tukio hili muhimu kwa mwenzake wa Karagwe.


Askofu Bagonza amemwelezea Kardinali Rugambwa kama mtu mwenye hekima kubwa, mnyenyekevu lakini hodari, mwenye nidhamu bila woga. Amesisitiza umuhimu wa kumuombea Kardinali Rugambwa katika majukumu yake mapya kama Mshauri wa Baba Mtakatifu. Historia hii imeweka alama ya utukufu na umoja wa dini, ikionyesha umuhimu wa mtamgamano katika uongozi wa Kanisa. Tutakua tunafuatilia kwa karibu jinsi Kardinali Rugambwa atakavyotekeleza wajibu wake katika nafasi hii mpya na kubwa ya uongozi katika Kanisa Katoliki.

0 Comments:

Post a Comment