TCRA WAONGOZA KUTOA GAWIO, RAIS AWAPA TUZO

 

MAMLAKA ya Masiliano nchini, (TCRA), imeng'ara katika kikao kazi cha Wenyeviti na Watendaji wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Taasisi za umma ambazo si za kibiashara lakini zinakusanya mapato kwa mwaka 2022/2023.



 Tuzo hiyo imetolewa leo Agosti 19,2023 jijini Arusha na Rais, Samia Suluhu Hassan mara baada ya kufungua kikaokazi hicho cha siku tatu kinachotatajiwa kumalizika jumatatu Agosti 21,2023.

Tuzo hiyo amepewa mwenyekiti wa bodi, Khalifan Saleh na mkurugenzi Mkuu, Dk Jabir Bakari.



Msajili wa Hazina, Nehemiah   Mchechu amesema kuwa TCRA imetoa gawio  la shilingi bilioni 272.4 kwa mwaka unaoishia juni 2023 huku akiwashukuru sana kwa utendaji wao mzuri.



Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Jabir amesema kuwa hakujua kama kutakuwa na tuzo hizo hivyo anafarijika kuona kuna watu wanafuatilia utendaji kazi wao.

"Ila tuzo hiyo ni kwa wafanyakazi wote wa TCRA  ambao wanafanya kazi kwa umoja,  bidii na ubunifu mkubwa unaotokana na maboresho makubwa ambayo tunaendelea kuyafanya ndani ya taasisi yetu," amesisitiza Jabir.

kiongelea mkutano huo, Jabir amesema kuwa maboresho yanayojadiliwa kwenye kikao kazi hicho anaamini yataleta mabadiliko makubwa sana kwenye taasisi za umma hapa nchini.

0 Comments:

Post a Comment