WANANCHI WA VIJIJI VYA CHEMCHEM NA MIKOCHENI WAIMWAGIA SIFA SERIKALI

 

Na Gift Mongi,MOSHI.




ADHA waliyokuwa wakiipata wananchi wa vijijin vya Mikocheni na Chemchem katika halmashauri ya wilaya ya Moshi mkoani kwa kukosa mawasiliano ya barabara sasa yametatuliwa na serikali ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan


Haya yanaelezwa na wakazi wa vijiji hivyo kufuatia ziara ya mwenge wa uhuru uliofika katika eneo hilo kwa ajili ya uzinduzi wa barabara hiyo.



'Kipekee tunashukuru rais Kwa kusikia kilio chetu kupitia kwa mbunge wetu Prof Patrick Ndakidemi ambapo mara kadhaa alikuwa akiipigia kilele'anasema Rose Mchau


Ameongeza kuwa  walisema kuwa, Kwa kipindi cha mvua vijiji hivo vilikuwa vikigeuka kuwa kisiwa kutoka na barabara kushindwa kupitika kutokana na maji.




Kwa upande wake Jonathan Mallya amesema kuwa, kwa sasa Seririkali imeonyesha kuwajali wananchi wa kata ya Arusha chini kwa vitendo kwa kujenga barabara ya TPC ambayo itakuwa ikipitika kipindi chote cha mvua na kiangaza.


'Tunamshukuru  mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele kupambana kuhakikisha matatizo yanayowakabili wananchi wake yanapatiwa ufumbuzi,'Anasema Mallya



Katika hatua nyingine Brenda Shuma anasema kwa.sasa.changamoto waliyko nayo ni ukosefu wa maji safi na salama hivyo kutumia wasaa huo kumuomba mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi kuona njia sahihi za kufikisha kilio chao.

0 Comments:

Post a Comment