Ahadi hizo zilitolewa
na Hayati Rais John Magufuli na Rais Samia Suluhu Hassan kwa
nyakati tofauti wakati waliposimama kusalimia wananchi kwenye eneo la
Kikatiti wakiwa njiani kuelekea jiji Arusha.
Waziri Mkuu Majaliwa leo Jumanne, JUni 20,2023 wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye jubilee ya
miaka 40 tokea kuanzishwa kwa chuo cha Biblia Sakila kinachomilikiwa na
Kanisa la International Evangelism Church (IEC) ambacho kinatoa elimu
bure ambapo zaidi ya wainjilisti, wachungaji na maaskofu 10,000 wamehitimu
kwenye chuo hicho tokea kianzishwe.
Amesema kuwa
serikali inatambua mchango unaotolewa na Askofu Mkuu wa IEC,
Dk Elihudi Isangya kupitia miradi ya maendeleo anayotekeleza kwenye
mikoa ya Arusha na Manyara katika sekta za elimu, afya, maji na maendeleo
ya jamii.
Waziri mkuu waliwaagiza
TARURA mkoa wa Arusha na wilaya ya Arumeru wakutane mara baada ya yeye kuondoka
Arusha ili wajadiliane namna ya kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo kutoka Kikatiti mpaka Sakila yenye kilometa sita.
Aidha alimuagiza
meneja wa shirika la umeme nchini, (TANESCO) mkoani Arusha abaki kwenye chuo
hicho pindi yeye na msafara wake unapoondoka ili aweze kupatia ufumbuzi wa
suala la kukatika umeme mara kwa mara kwenye eneo hilo.
"Kabla sijaendelea na mazungumzo haya jana (Juni 19,2023) nilienda kumuaga kiongozi wangu mkuu, Rais, Samia Suluhu Hassan nikamwambia nakuja Sakila... akasema niliwahi kusimama barabarani pale Kikatiti mikaahidi ujenzi wa barabara ya kuelekea Sakila hivyo amenituma kuleta salamu kwenu," alisema Majaliwa na kuongeza.
...Kwanza anawapongeza kwa kuifikia hii miaka 40 kwa mafanikio makubwa sana. Ameniagiza nipokee changamoto zote na nizifanyie kazi hivyo namezipokea na nyingine nitazifanyia kazi hapahapa," .
"Nimefurahi
kusikia idadi kubwa ya wahitimu zaidi ya elfu 10 katika kipindi cha miaka 40
mbao kwa sasa wengine ni maaskofu, wachungaji na wainjilisti ama kwa hakika
mmeweza kujitengenezea na kujiwekea akiba kwenye kazi ya Mungu,".
"Mmetusaidia sana serikali hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na mmomonyoko wa maadili na chuo kimejikita kwenye kuhimiza imani kwa kuwa na somo la matendo ya huruma na amani. Wahitimu tumieni elimu hiyo kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla,".
Aidha Waziri Mkuu
Majaliwa amewapongeza kwa hatua yao ya kujiwekea malengo ya kuwnza ujenzi wa
chuo kikuu kitakachotoa elimu kwa wananchi wote ikiwa ni mwendelezo wa mchango
wa kanisa hilo kwa jamii.
"Kwa miaka 20
mmekuwa mkitoa huduma ya kuchimba maji bure kwenye maeneo mbalimbali ....Sisi
kwa upande wa serikali mnapoamua kuwekeza kwenye miradi ya maji tunawaona
mkiunga mkono mpango wa serikali wenye kauli mbiu ya kumtua ndoo mama,"
alisema Waziri Mkuu.
Alisema
kuwa IEC imejenga zahanati inayotoa huduma bure kwa jamii ya
wananchi wanaoishi Sakila ambayo wanataka kuiboresha ili ifikie hadhi ya hospitali , chuo cha ufundi Maji ya Chai, shule ya
awali, shule ya msingi SLUYS na sekondari ya Hebron yenye kutoa elimu mpaka
kidato cha sita.
"Chuo hiki
kimechimba maji kwenye maeneo mengi bila kudai chochote mfano kwenye uwanja wa
Sheikh Amri Abeid (Arusha), katika shule za msingi na sekondari Sinoni
Unga Limitedi jijini Arusha, kituo cha walekavu Usa River na kwenye
hospitali ya wilaya ya Arumeru," alisema Dkt Maasa ambaye pia ni
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Maridhiano na Amani nchini.
Amesema kuwa
wamechimba maji kwenye eneo la Ngaramtoni na Mringaringa na na
kufunga mtambo wa solar hivyo wananchi wanapata maji bila shida yoyote.
Dkt Maasa amesema kuwa
Chuo kimekuwa mdau katika ujenzi wa zahanati wilayani Simanjiro na wamechimba
visima vinne na kufunga mitambo ya umeme wa sola hivyo maji yanapatikana bila
shida yoyote.ì
Hata hivyo amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ubovu wa barabara kutoka barabara kuu ya Moshi Arusha mpaka chuoni hapo ambayo imejengwa kwa kiwango cha changarawe lakini haipitiki kirahisi.
“ Barabara ni
changamoto na hili tunafurahi kwamba umepita umeiona. Kutoka Kikatiti
mpaka Sakila ambayo Rais wa awamu ya tano John Magufuli aliposimama katika eneo
la Kikatiti akielekea Arusha aliahidi kuijenga na mama Samia (Rais Samia Suluhu
Hassan) alisimama hapo alipokumbushwa alisema inawezekana,” alisema Dkt Maasa
Changamoto nyingine aliyomweeza Waziri Mkuu ni ya umeme kukatika mara kwa mara kwenye eneo hilo linalotumiwa na wanachuo na wakufunzi wao pamoja shule za awali, msingi na sekondari pamoja zahanati ya afya.
Amesema kuwa IEC wanatoa huduma ya kusaidia wazee kwa kuwapa chakula na huduma za afya huku wakiwa na kituo cha watoto yatima ambacho huwapatia huduma zote muhimu ambapo watoto hao mbali ya chakula,mavazi, malazi na matibabua pia hupatiwa elimu kuanzia shule ya awali sekondari na chuo cha ufundi kwenye shule za kanisa hilo.
IEC pia inamiliki kituo Kituo cha radio cha New Life kinachotoa elimu kwa jamii sanjari na kueneza neno la Mungu na huduma ya maombi makanisa mengi yameanzishwa na waliohitimu katika chuo hicho.
Naye, kofu wa Kanisa la International Evangelism la nchini Congo, Askofu Byamungu Magala ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu.
0 Comments:
Post a Comment