WANACHI WA NGORONGORO WAWABURUZA KORTINI NCAA, MKURUGENZI WA WANYAMAPORI


RUFAA ya wananchi wa Ngorongoro kupinga faini  ya mifugo inayotozwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, (NCAA), waliyodai taasisi hiyo  haina mamlaka hayo kisheria imeahirishwa mpaka Mei 10, 2023 kwa ajili ya kusikilizwa.


Rufaa hiyo ya Jinai namna 9/ 2023 imekuja mahakamani Kuu Kanda ya Arusha, leo, Aprili 5, 2023 mbele ya Jaji, Mohamed Gwae kwa ajili ya kutajwa.


Waleta rufaa katika shauri hilo,  Rafaeli Oloishiro  na Baraka  Kesoi ambao wote ni wakazi wa Ngorongoro anawakilishwa na mawakili, Joseph Oleshangay na Denis Mosses.

Upande wa wajibu rufaa NCAA, Mkurugenzi wa wanyamapori na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG), wanawakilishwa na mwanasheria wa serikali, Tony Kiloma.


Wananchi hao wa Ngorongoro wanaiomba mahakama itengue utozaji wa faini ya shilingi laki moja kwa kichwa cha ng’ombe kwa kile wanachoeleza kuwa ni batili na ni kinyume cha sheria.

Wameeleza kuwa NCAA haina mamlaka ya kutoza faini kwenye sehemu ambazo zimeanzishwa na Sheria ya Wanyama Pori, Sura 283 ambapo mwenye mamlaka ni mkurugenzi wa wanyamapori.

Katika ombi la tatu, waleta rufaa hao wanapinga tozo ya  faini ya shilingi 25,000 kwa kondoo kwa kile wanachoeleza kuwa ni batili na ni kinyume cha sheria huku wakieleza kuwa kutoza faini ya 13,000,000 ni kinyume cha kiwango kilichowekwa na sheria.



Jaji  Gwae, ameahirisha kesi hiyo  hadi Mei 10,2023.



0 Comments:

Post a Comment