WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Arusha, wamemchagua Namelok Sokoine kuwa mwakilishi wa mkoa huo katika nafasi ya NEC Mkoa kuwakilisha chama hicho taifa baada ya kuwashinda wagombea wenzake 9.

Akitangaza matokeo hayo leo , Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda alimtangza Namelock Sokoine kwa kupata kura 39 na kumwangusha mpinzani wake wa karibu mfanyabiashara, Hussein Gonga aliyepata kura 16.


Pinda alisema kuwa  wajumbe waliopiga kura walikuwa 67 na nafasi ya tatu ilishikwa na Daniel Palangyo alikuwa akitetea nafasi ya NEC kwa kupata kura 5, nafasi ya nne ni Judith Mollel aliyepata kura 3, Elibahati Lowassa na David Lemilla waliopata kura 2 na wagombea wengine Novatus Makunga, Prof. Samweli Ilila na Abdullazi Mawia hawakupata kura.




















Pinda ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa Arusha, amewataka wajumbe kumpa ushirikiano Namelok katika kuifanya kazi yake vizuri na kuacha kumvua shati, kwani hiyo sio stahili ya uongozi ndani ya chama.

Namelok amewataka wana CCM kuvunja makundi kwani CCM ni moja na kundi lililobaki ni moja la Chama Cha Mapinduzi na sio vinginevyo.






 Naye Gonga aliwashukuru viongozi wa chama kwa jinsi walivyoendesha uchaguzi wa wazi na huru na yote aliyotaka kuyafanyia kazi iwapo angeshinda sasa atayapeleka kwa Namelok na atashirikiana naye kwa hali na mali ikiwemo suala la kutengeneza ajira kwa vijana na kina mama.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen aliwataka wana CCM kumpa ushirikiano Sokoine na kusema kuwa kilichobaki ni kuijenga CCM na sio vinginevyo.