TANZANIA YATOA MSAADA KWA UTURUKI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa kibinadamu kwa Serikali ya Jamhuri ya Uturuki kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo tarehe 6/02/2023 na kusababisha madhara makubwa kwenye miji ya Kusini Mashariki mwa Uturuki .


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Lt Jen (Mst) Yacoub Hassan Mohammed,  alikabidhi msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Bw. Muhammet Maruf Yaman, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Taasisi inayohusika na majanga (AFAD) alipokea kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Uturuki.


Balozi Jenerali Mohamed alitumia fursa hiyo kuwasilisha pia salamu za pole kutoka kwa  Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya   Tanzania pamoja na Watanzania kwa ujumla kwenda kwa  Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki na Raia wa Uturuki kufuatia madhara yaliyosababishwa na tetemeko hilo.

0 Comments:

Post a Comment