KESI YA LOLIONDO VIGOGO WAITWA MAHAKAMANI

 MAHAKAMA Kuu  Kanda ya Arusha imetoa amri ya kufika mahakamani kwa wajibu maombi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,(IGP), Mkuu wa mkoa wa Arusha na wenzao wanne kwenye kesi ya kulazimishwa kupotea ( Enforced disappearance), kwa mzee Oriais Oleng’iyo, (85) wa Ololosokwan, Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro



Wajibu maombi wengine ni  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamanda wa Polisi Mkoa, (RPC)  wa Arusha,  Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro na  Mkuu wa polisi wilaya wa wilaya hiyo.



Amri hiyo imetolewa leo Machi 22,2023 na Jaji Mohamed Gwae  anayesikiliza maombi hayo namba  68/2022 yaliyokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kuendelea baada ya wajibu maombi hao na mawakili wao kutokutokea mahakamani bila taarifa.



Pia mahakama hiyo imewaagiza mawakili wa mleta maombi, (jina lake halikutajwa) kuja na mteja wao ambaye ni  mtoto wa Mzee anayedaiwa kutoonekana siku kesi hiyo itakapokuja tena


Mawakili wa mleta maombi ni Joseph Shangai, William Ernest na Simon Mbwambo  

 



Awali Upande wa waleta maombi wanaiomba mahakama hiyo iamuru wajibu maombi  kumleta mahakamani Oriaisi Ng’iyo ambaye amepelekwa kusikojulikana tangu alipokamatwa nyumbani kwake Engong’u Nairowa, Kata ya Ololosokwan, Loliondo wilaya ya Ngorongoro.

 

Pia wanaiomba  Mahakama iamuru au kuwaelekeza wajibu maombi kumwachia huru Oriasi Pasilange Ng’iyo Kurosawa alikoshikiliwa tangu Juni 10, 2022 na  iamuru walalamikiwa waje mahakamani kueleza sababu za kumshikilia Oriasi Pasilange Ng’iyo kinyume cha Sheria.

 

Katika ombi lingine wanaoimba mahakama iamuru na kuelekeza wajibu maombi kuleta mwili wa Oriaisi Ng’iyo akiwa hai au asipokuwa hai.



 Jaji Gwae aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 30 mwaka huu  kwa ajili ya kusikilizwa.

 

 

 


 

0 Comments:

Post a Comment