MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 8



MFANYAKAZI wa hoteli, Kelvin Julius Abraham, (19) amefikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Arusha akikabiliwa na mashitaka mawili ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka nane.


Aidha imedaiwa kuwa Kelvin alimbaka na kumlawiti mtoto huyo mara nyingi  ambapo alikuwa akimtishia kumchoma kwa kisu endapo atasema kwa mtu yetote.

Mkazi huyo wa Kiding'a amesomewa maelezo ya awali leo na Wakili wa Serikali, Neema Mbwana mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi, Bittony Mwakisu wa mahakama ya wilaya Arusha.

Wakili Neema aliieleza mahakama hiyo kuwa Kelvin anadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya mwezi Agosti na septemba 5, 2022.

 Katika kosa la kwanza imedaiwa kuwa katika maeneo ya Ilboru ya juu katika jiji na wilayani Arusha (Kelvin) alifanya mapenzi na mtoto wa miaka nane kinyume cha maumbile kinyume cha sheria.

Katika shitaka la pili Kelvin anadaiwa kumbaka mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka nane  kinyume cha sheria.

"Mhanga ni mtoto wa miaka nane ni mwanafunzi. Mnamo
Septemba 5, 2022 mama wa mtoto alisikia mtoto analalamika sehemu za haja kubwa zinamuuma ambapo alipomuuliza ndipo mtoto alimweleza kuwa  Kelvin (alikuwa akimlawiti) kisha anampa shilingi 500 huku akimwambia asimwambie mtu akisema atamchona kisu," alieleza wakili wa serikali, Neema na kuongeza. 

... Mtoto alisema kuwa Kelvin amekuwa akimwingilia kinyume na maumbile mara nyingi ambapo mara ya mwisho ilikuwa septemba 5, 2022,".

"Mama alimkagua mtoto,  ambaye alipomshika sehemu za siri mtoto alilamika kuwa ana maumivu makali hivyo alienda kutoa taarifa polisi wakapewa PF 3 wakaenda hospitali kufanyiwa ukaguzi wa kitababu,".

"Matokeo ya kitabibu yalionyesha mtoto ameingiliwa na kinyume na maumbile na sehemu ya mbele yaani alibakwa na sehemu ya nyuma yaani kulawitiwa,".

Wakili wa Serikali, Neema ameieleza mahakama hiyo kuwa baada ya taarifa hizo mshitakiwa alitafutwa na kukamatwa ambapo yupo mahakamani hapo kwa ya  kujibu mashitaka yanayomkabili.


Alisema kuwa wanatarajia kuleta mashahidi wanne, vielelzo viwili cheti cha kuzaliwa cha mhanga na fomu ya polisi PF  3.

Hakimu Mkazi Mfawidhi,  Mwakisu aliahiridha shauri hilo mpaka Februari 1, 2023 ambapo shauri hilo litakuja kwa ajili ya upande wa jamhuri kuleta mashahidi wao.

 



0 Comments:

Post a Comment