BRELA NA NIDA KUBORESHA HUDUMA

  Na Mwandishi wetu- Dodoma



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya amesema uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) zitasaidia wananchi kupata huduma mbalimbali na wawekezaji kuwekeza kwa wingi Nchini.


Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo  Jijini Dodoma  wakati wa kikao cha Makatibu na Wakuu wa Taasisi kujadili utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA).



Mmuya amesema  kutatuliwa kwa changamoto zinazokabili mamlaka hizo kunatoa fursa kwa wafanyabiashara  kuanzisha bishara zao, viwanda kwa mujibu wa sheria hivyo kuongeza pato la mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA),  Godfrey Nyaisa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho .



Mkurugenzi wa Mipango na Milki  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Deusdedit Buberwa (wa kwanza kushoto) akichangia hoja wakati wa mjadala huo anayefuata ni Mkurugenzi wa Sheria (NIDA) Bwa. Shani Mayosa katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.


(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

0 Comments:

Post a Comment