WANYAMAPORI walio kwenye eneo la ikolojia ya hifadhi za Taifa ya Tarangire na Manyara wapo hatarini kupungua kwa magonjwa baada ya kaya zaidi ya 300 kuishi katika eneo hilo na hivyo kuzuia wanyama kutembelea.
Afisa Maliasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Michael Gwandu, amesema kaya hizo zimebainika katika uhakiki wa eneo hilo, uliofanywa na Taasisi ya utafiti wanyamapori(TAWIRI)Mamlaka ya wanyamapori(TAWA) na watendaji wa serikali mkoa wa Manyara.
“baada ya kubainika tatizo hili hivi sasa tathmini inaendelea ili hatua zichukuliwe katika kuhakikisha eneo hilo linalindwa kwani kama mapito hayo yakizibwa kabisa wanyama wanaweza kuathirika na magonjwa hadi kufikia kufa”alisema
Gwandu amesema ni muhimu mapito hayo, kubaki wazi ili kuwezesha wanyama kuweza kutembelea kuzunguka ikolojia hiyo,ambayo huwezesha kupata uzao tofauti na hivyo kupunguza athari za kuzaliana familia moja .
“ni muhimu sana kulinda ikolojia hii kwani wanyama wanaotoka Tarangire ndio wanaozunguka hifadhi ya Manyara, Ngorongoro,mapori ya akiba ya Mkungunero na maeneo mengine hivyo tunatoa wito watu kuacha kuvamia maeneo haya”amesema
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TAWA Kanda ya Kaskazini,Peter Mbanjoko amesema uvamizi katika maeneo ya mapito ya wanyamapori umekuwa na athari katika uhifadhi na kuchochea ujangili.
“kuna changamoto ya uvamizi katika eneo la ikolojia ya Tarangire- Manyara na ndio sababu kumekuwepo na ujangili na migogoro ya wanyama kula mazao kwani kuna watu wamelima katika maeneo ya ya mapito ya wanyamapori”alisema
.jpeg)
0 Comments:
Post a Comment