"Tumekutana katika ukumbi wa Mlimani City jijini kujadili tulipotoka, tulipo na mahali tunapotaka kwenda, Agosti 03, 2020 ndio ilikuwa mara ya mwisho kukutana hapa kwa ajenda moja maalumu ya kumpitisha mgombea wa Urais wa chama chetu"
"Kwa miaka zaidi ya 25 tumeijenga @ChademaTz tofali kwa tofali hadi leo kuwa chama tumaini kwa uhuru, haki na maendeleo ya watu"
"Hatupaswi kulia na kulalamika, siku zote nahubiri kwenu kuwa hatupaswi kujenga kisasi wala chuki bali tuwe na nguvu na shauku ya kukijenga chama chetu"
"Mwaka 2020 hatukuibiwa kura bali tuliibiwa mfumo wa uchaguzi, wakati binadamu tunalalamika na yanayotusibu, Mungu ana njia zake za kuonesha ukuu wake. Yaliyotokea mwaka 2021, yalipaswa kutokea ili kudhihirisha ukuu wa Mungu katika maisha yetu"
"Ilibidi Mbowe na wenzake waishi gerezani ili kuibua mijadala ya ndani na nje ya nchi katika haki na usawa, ilibidi Mbowe akamatwe ili dunia ivijue vyombo vyetu vya dola"
"Baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 tumeona mserereko wa watu wengi wakiongezeka katika kudai haki"
"Kama hatufahamu, huko nje umma uko uko tayari kwa mabadiliko kuliko hata hamasa ya mabadiliko tuliyo nayo viongozi"
"Nawashukuru viongozi wote wa vyama vya siasa kwa kunisapoti nilipokuwa gerezani, pamoja na tofauti zetu ndogo ndogo lakini sote tunabaki kuwa wamoja
"Wakati nipo gerezani nilikuwa nakaa na kujiuliza hivi mimi Mbowe ni nani hata watu wafunge, kuomba na kujitolea kuhusu mimi. Wapo waliotoa fedha na kusaidia familia zetu hata kuwapa faraja familia zetu. Nasema nawashukuru sana"
"Nawashukuru viongozi na wanachama wa CHADEMA, walidhani kwamba kesi ile ingetubomoa imetujenga na kuwa imara zaidi ya jana. Nawashukuru sana lakini pia niwashukuru sana Tanzania"
"Nilivyopata mwaliko kwenda Ikulu sikujitia kiburi kukataa. Wajibu wangu kama kiongozi ni kuweka vitu vingine chini ili kusimamia maslahi na masuala ya kuinua Taifa hivyo nilikwenda Ikulu"
"Nilimwambia Rais, Samia Suluhu kuna mambo mengi ambayo kama taifa yanatutenga, na kutengeneza matabaka ya raia daraja la kwanza na raia daraja la pili na swala hili halipaswi kuendelea"
"Nilimwambia Rais @SuluhuSamia kuwa Serikali imekuwa ikihubiri amani, amani huku mkisahau msingi mkuu wa amani nao ni haki"
"Nimechoka kuona viongozi wangu wakipelekwa gerezani, sio sifa kuona vijana wa Chadema wakikamatwa, nilimwambia Rais @SuluhuSamia kuwa tujenge misingi ya kuaminiana"
"Niliamini katika kukutana ili kuliponya Taifa na kama njia ya kumaliza tofauti zetu"
"Nafasi ya chama chetu leo ni chama kikuu cha upinzani nchini, haina maana nafasi hiyo tukawa nayo siku zote, inawezekana kesho chama kikuu cha upinzani kikawa @ACTwazalendo, NCCR, CUF. Hivyo isiwe sababu ya kudhalilisha vyama vingine, hili ni lazima liachwe"
"Ziara yangu kwenda kwa Rais Suluhu sio tukio la miujiza, na inaonekana hivyo kwa sababu tumejenga utamaduni wa kutoaminiana"
"Tuko tayari kutoa ushirikiano kwa ofisi ya msajili na kuendelea kuwa na ushirikiano wa vyama vingine vya siasa, lakini pia ofisi ya msajili mtuache huru tufanye siasa zetu na sio kutupangia namna ya kufanya siasa"
"Hata ukienda kwenye mataifa yaliyopigana kwa ajili ya ubaguzi, na hata Mandela alipokuwa jela bado alifanya mazungumzo, tukitaka kuliponya Taifa hili, CHADEMA hatuwezi kuliponya peke yetu ni lazima tuwalete watu wote pamoja wa vyama vya siasa na wasio na chama"
"Nilimuhakikishia Rais,Samia kuwa sisi Chadema, hatutaacha ajenda yetu ya katiba, na nilimwanbia tunasikitika sana suala la katiba kuliona sio la wakati huu na pia nilimuuliza mnaogopa nini katika katiba?"
"Tunataka katiba na kama tunabishana kuhusu katiba basi tubishane kwa hoja kuhusu maudhui yanayopaswa kuwemo kwenye katiba. Sisi CHADEMA pekee hatuwezi kutengeneza katiba, hivyo hivyo kwa CCM na vyama vingine, ni lazima tuungane wote ili kupata katiba"
"Hatuwezi kuwa na katiba ambayo kila tunachokitaka CHADEMA basi ndio kiwe, hivyo hivyo hatuwezi kuwa na katiba ambayo vyama vingine na watu wengine kila wanachotaka ni lazima kiwe, ni lazima tujadiliane na kukubaliana"
"Tutaheshimu serikali na chama chake kama na wao pia watatuheshimu lengo likiwa ni kujenga jamii na nchi isiyo na matabaka ya watu"
"Ajenda ya tume huru ni ajenda yetu sote, lakini ajenda ya tume huru haipaswi kusimamisha mchakato wa katiba mpya, haya mambo yanapaswa kutegemeana na kwenda pamoja"
"Pamoja na uchumi wa nchi yetu kukua lakini wananchi wameachwa nyuma na ukuaji huo wa uchumi, uchumi a unakuwa kwa makampuni makubwa huku Watanzania wakiendelea kuwa mafukara katika uchumi huo unaotajwa kuku"
"Kila kitu leo tunaisingizia Corona (ugonjwa wa Uviko-19) na vita vya Ukraine na Urusi, kimsingi sisi hatukuathirika na Uviko-19 kwa kuwa hatukujifungia ndani"
"Hatuwezi kuwa na uchumi endelevu katika nchi kwa kuwatoza watu wa hali ya chini tozo na kodi, tena watu ambao wanapambana kila siku kupata mlo wa siku moja"
"Tulivyoacha kupokea ruzuku walidhani tusingeweza kujiendesha hata kwa mwezi mmoja, walidhani kwamba ChademaTz inajiendesha kwa ruzuku pekee ya serikali bila kusahau CHADEMA inaendeshwa kwa akili, maarifa na upendo"
"Jambo moja kuu linalosubiriwa leo na watu wengi, wana CHADEMA na wasio wana CHADEMA ni rufaa za waliokuwa wanachama wetu 19, tuliwaita na wote wameitikia wito, tunavyoongea sasa wapo katika viunga vya Mlimani City"
"Lazima tukihami chama chetu kwa wivu na nguvu kubwa nyakati zote, na hata Baraza Kuu litakapoisha tutoke tukiwa tuko vizuri, tuna nguvu zaidi na kuona fahari ya chama chetu"

0 Comments:
Post a Comment