MAWAZIRI WATANO WAKUTANA KUJADILI ANWANI ZA MAKAZI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi.



Kikao hicho kimefanyika leo Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri wanne.

Mawaziri hao ni pamoja na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Hamza Hassan Juma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.


Kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti  2022 nchini  ambapo itakuwa Sensa ya Sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na  sensa ya watu na makzi hufanyika  kila baada ya miaka 10.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Innocent Bashungwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.



Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akichangia hoja wakati wa kikao cha mawaziri cha  kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika  Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dodoma.



Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Nape Nnauye akieleza jambo katika kikao cha mawaziri cha  kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika  Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dodoma.



Mkurugenzi wa Mawasiliano  Wazara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Clarence Ichwekeleza akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika  Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dodoma.


(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

0 Comments:

Post a Comment