URUSI ILIVYOISHAMBULIA UKRAINE KWA MAKOMBORA KWA SAA 15 MFULULIZO

 


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwataja watu wake kuwa "ishara ya kutoshindwa".

Jiji la Mariupol, kusini mashariki, imeshambuliwa kwa makombora leo Jumatano, naibu meya wake Sergiy Orlov aliambia BBC.

"Hali ya Mariupol ni mbaya, tunakaribia kukumbwa na janga la kibinadamu. Tumeshuhudia zaidi ya saa 15 za mashambulizi ya makombora bila kusitishwa," alisema.

"Jeshi la Urusi linafanyia kazi silaha zake zote hapa - mizinga, mifumo mingi ya kurusha roketi, ndege, roketi za mbinu. Wanajaribu kuharibu jiji."

Bw Orlov alisema vikosi vya Urusi viko kilomita kadhaa kutoka mji kwa pande zote, na mashambulio dhidi ya miundombinu muhimu yamekatiza huduma za maji na usambazaji wa umeme katika maeneo ya jiji.

"Hatuwezi kukadiria idadi ya wahasiriwa huko, lakini tunaamini angalau mamia ya watu wamekufa. Hatuwezi kuingia kuchukua miili," alisema. "Baba yangu anaishi huko, sina uwezo wa kumfikia, sijui yuko hai au amekufa."

Huduma za dharura za Ukraine zilisema zaidi ya raia 2,000 wameuawa kufikia sasa katika uvamizi wa Urusi, ingawa BBC haikuweza kuthibitisha idadi hiyo. Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne kwamba takriban raia 136 wameuawa, ikifikiri kwamba inakadiria kwamba idadi halisi ya watu waliouawa ni kubwa zaidi.

Rais Zelensky awali alisema kwamba Urusi inajaribu "kufuta" historia ya nchi yake.

Chanzo BBC

0 Comments:

Post a Comment