TAARIFA YA KAMATI KUU YA CCM YAMUIBUA MAKONDA

 


WAKATI Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ikiiielekeza serikali kuangalia upya mwenendo wa jeshi la polisi nchini ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameibuka na kusema yuko tayari kutoa ushirikiano kubainisha polisi wanaolinda wafanyabiashara matapeli.



Taarifa ya hiyo imetolewa leo Machi 12, 2022, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar es Salaam, ambapo pia kamati hiyo imempongeza Rais Samia kwa hatua alizozichukua kufuatia mauaji yaliyofanyika mkoani Mtwara na Tanga.

"Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imeielekeza serikali kuangalia upya mwenendo wa jeshi la polisi nchini ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maafisa kinyume na miongozo ya utendaji wa kazi," amesema Shaka.

Muda mfupi baada ya taarifa hiyo ya CCM, akaibuka Makonda , kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema yupo tayari kutoa ushahidi mbele ya kamati hiyo.

Makonda ambaye kuwa kimya kwa muda mrefu huku akiandamwa na mzimu wa kutaka ashtakiwe leo ameamua kuvunja ukimya Kwa kuandika juu ya uonevu unaofanywa na Jeshi la Polisi.

"Naunga mkono hoja ya kamati kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi, wanaolipaka tope jeshi la polisi kwakuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi PAUL MAKONDA niko tayari kutoa ushirikiano," unasomeka ukurass huo wa  Makonda kwenye mtandao wa Instagram.


0 Comments:

Post a Comment