SAMIA AMRUDISHA MCHECHU NHC, AMPELEKA POLEPOLE UBALOZINI

 



RAIS, Samia Suluhu Hassan amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) huku mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole akiteuliwa kuwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.


Aidha, Peter Ulanga ameteuliwa kuwa  Mkungenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL).

Taarifa ya uteuzi ya Ikulu imesema kuwa Rais Samia pia amemteua aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.

Nahodha pia ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar na mwaka 2015 alikuwa mtia nia ya kugombea Urais kupitia CCM.

Katika uteuzi huo, Rais Samia amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe kuchukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya anayestaafu.

Pia Rais Samia amewateua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (mstaafu), Ernest Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi mstaafu wa Takukuru kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL)

 

0 Comments:

Post a Comment