WATALII 900 WA UKRAINE WAKWAMA ZANZIBAR

WATALII  zaidi ya 900 raia wa Ukraine  wamekwama Zanzibar baada ya muda wao wa kukaa visiwani humo kuisha huku wakikosa fedha za kuendelea kulipa hoteli.

Hata hivyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeingilia kati suala hilo na kuangalia njia bora ya kuwasaidia watalii hao.




Akitolea ufafanuzi jambo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 28, 2022 Ikulu ya Zanzibar, Rais Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali inafanya mpango kuhakikisha raia hao wanaendelea kuwa salama.



"Taarifa nilizonazo kuna watalii wa Ukraine kama 900 tisa hivi wapo Zanzibar na hawawezi kurudi kwao, wameomba msaada ili Serikali iwasaidie hawawezi kuendelea kukaa hotelini kwa sababu hawana fedha lakini tumeanza mazungumzo wale wenye hoteli pamoja na Serikali tunazungumza kuona kwa jinsi gani tutawasaidia.


"Tunaangalia namna ya kuwasaidia mpaka Serikali yao itakapopata uwezo wa kuleta msaada kwahiyo kuna makubaliano ambayo yameanza kuonekana na Hoteli kuwapa msaada bila ya kuwachaji lakini na Serikali kuwaangalia wale wenye hoteli kwa upande wa kodi kwahiyo tunazungumza, ukweli ni kwamba tunaona umuhimu wa kutoa msaada," amesema Rais Mwinyi.

0 Comments:

Post a Comment