WASANII WA HUBA WAENDA DUBAI

 

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, amewataka  wasanii na watengenezaji wa Tamthilia ya HUBA inayorushwa na DStv kuutangaza utamaduni wa Tanzania duniani ili wageni wengi watembelee nchi hiyo.

Amesema hayo leo Februari 12, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akiagana na kundi hilo lililoondoka kwenda  nchini Dubai kuandaa kazi zao.


Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuona filamu za Tanzania zinakuwa na ushindani katika  soko la kimataifa.



Katika tukio hilo  Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa wizara Dkt. Hassan Abbasi na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo ambao wote walizawadiwa  vyeti vya shukrani kwa  kutambua mchango wao kwenye tasnia ya Filamu.

0 Comments:

Post a Comment