NAPE TOENI TAARIFA WIZI WA BANDO

 

 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema wako tayari kushughulikia malalaamiko ya wizi wa bando ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa kupitia namba maalum za Mamlaka ya Mawasiliano nchini, (TCRA)

"TCRA wana namba ya bure popote ulipo namba ni hii 0800008272 unapiga popote bila malipo piga eleza kwamba umeibiwa bando lako na email @ dawatilahuduma  @tcra.go.tz,

Ameyasema hayo leo Februari 21, 2022 wakati akiwa kwenye mahojiano katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa Clouds FM.

‘Uchambuzi wetu unaonesha hasa Mitandao baadhi ya haya malalamiko sio ya watu wengi sana ni watu kadhaa ndio maana nikasema mwenye malalamiko kuhusu kuibiwa bando aje tupo tayari kumuhudumia na TCRA wana namba ya bure popote ulipo namba ni hii 0800008272 unapiga popote bila malipo piga eleza kwamba umeibiwa bando lako na email @ dawatilahuduma  @tcra.go.tz,” amesema  Nnauye.

0 Comments:

Post a Comment