Rais Uhuru Kenyatta amemunga mkono rasmi kinara wa chama cha ODM nchini Kenya Raila Odinga kuwania urais.
Akihutubia mkutano wa wajumbe katika eneo la mlima Kenya, Uhuru ameitaka jamii yake kumuunga mkono Odinga akisema kwamba anaheshimu maslahi ya taifa.
Kiongozi huyo bila kumtaja naibu wake William Ruto amesema kwamba hatakuwa na tatizo naye katika siku za usoni iwapo 'atabadilika'.
''Nawaomba mumuunge mkono Raila Odinga kwasababu anapigania maslahi ya taifa hili. 'Kijana wangu' atakapobadilika tutamfikiria pia naye'', alisema Uhuru.
Hii ni mara ya kwanza rais Uhuru Kenyatta ameiambia jamii yake hadharani kwamba kiongozi huyo wa chama cha ODM ndiye anayempigania kumrithi.
Rais Kenyatta amekuwa akiashiria kumuunga mkono kiongozi huyo wa ODM bila kumtaja moja kwa moja.
Katika Mkutano huo wa tatu wa Sagana, Uhuru alikuwa waziwazi akisema kwamba Raila ndiye bora sio tu kwa Mlima Kenya bali kwa Wakenya kwa jumla.
Rais amesema kwamba ameongeza uchumi wa taifa hili maradufu tangu alipochukua hatamu kutoka kwa rais Mwai Kibaki.
Alisema kwamba kiongozi huyo wa ODM anaelewa kule taifa linakoelekea hivyobasi atakuwa na amani kumpatia uongozi.
Chanzo BBC
0 Comments:
Post a Comment