WATU tisa wamefariki dunia na wengine sita kuokolewa wakiwa hai huku wengine zaidi ya kumi wakiwa hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama baharini katika Mkoa wa Kusini Pemba, Visiwani Zanzibar.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Thadei Mchomvu amethibitisha kwa shirika moja la habari kuwa ajali hiyo ilitokea jana jioni (Jumanne, Januari 4, 2022).
Alisema kuwa boti hiyo ilikuwa imebeba watu kati ya 30 na 40 wakitokea Chakechake kwenda msibani katika Kisiwa cha Panza na mpaka sasa chanzo cha ajali akijajulikana.
“Nahodha hajapatikana na hali ya hewa haikuwa mbaya hivyo hatujajua chanzo kamili maana inaonekana tatizo sio upepo,” Kamanda Mchomvu
Alisema zoezi la uokoaji litaendelea leo Jumatano asubuhi baada ya jana zoezi kusitishwa kwa sababu ya giza.
0 Comments:
Post a Comment