SAKATA la mwanamke ,Teddy Malya, (31)kuuawa na hawara na kisha mwili wake kukutwa umetupwa kwenye shamba la migomba ukiwa utupu limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi kumkmta mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye inadaiwa amekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mwili huo ulipatikana maeneo Ilboru Kisiwani, wilayani Arumeru Mkoani Arusha anakoishi marehemu majira ya saa 2:30 asubuhi na wapita njia ambapo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mt Meru.
Mwanamke huyo anadaiwa kutoonekana siku moja kabla ya mwili huo kugundulika na wapita njia ukiwa kwenye shamba hilo la migomba huku majani yakiwa yamevurugika .
Taarifa za wakazi wa eneo hilo zimedai kwamba marehemu alikuwa na mahusiano ya siri na mwanaume mwingine ambaye anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kwa kuwa inadaiwa alikuwa na ugomvi akimtuhumu marehemu kutoa ujauzito wake, Jambo ambalo Mme wa marehemu alikanusha.
Mme wa marehemu, Richard Lanyuni(42) alieleza kuwa aligundua mke wake kuuawa baada ya kupokea taarifa za wapita njia kuwa kuna mtu amelala kwenye shamba la migomba ndipo alipofika na kuukuta ni mwili wa marehemu mkewe akiwa amepoteza maisha.
Akihojiwa na waandishi wa habari Lanyuni alieleza kwamba marehemu mkewe ambaye hufanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya Mbege hakuonekana kurejea nyumbani mida ya kawaida na ilipotimu majira ya saa saba usiku aliamua kulala ndipo kesho yake alipata taarifa za mkewe kuuawa.
“Mke wangu anafanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji siku hiyo hakurejea nyumbani lakini nimeambiwa siku ya tukio alionekana akiwa na kijana mmoja anayefahamika.kwa jina moja la Baraka,”alisema Lanyuni na kuongeza.
.....Kuhusu mke wangu kuwa na mahusiano na mwanaume huyo siwezi kujua Ila hakuwa na ujauzito Ila naomba vipimo vya kitaalamu vifanyike kujua kama kweli alikuwa na ujauzito maana anashughuli zake mimi siwezi kumchunguza sana.
Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani hapa, (RPC) , Justin Masejo amesema kuwa wanamshikilia mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume (jina limehidhadiwa kwa ajili ya uchunguzi) Kwa tuhuma za kumuua mwanamke huyo.
Amesem kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa amekiri kuhusika na tukio hilo akidai kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu na siku ya tukio waliokuwa pamoja kwenye pombe na kulitokea ugomvi wa kutoelewana .
“Mpaka Sasa tunamshikilia mtu mmoja ambaye amekiri kuhusika na mauaji hayo lakini tunaendelea na upelelezi ili kujiridhisha zaidi kama mhusika ni yeye peke yake ama kuna wengine”alisema Kamanda.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiroriki, Emmanuel Lazaro akidai kwamba mtuhumiwa alikuwa anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu enzi za uhai wake na siku ya tukio walionekana wakiwa pamoja wakinywa pombe.
Mwenyekiti huyo alieleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na baadhi ya nguo zake na viatu kukutwa eneo la tukio Jambo ambalo waliamini anahusika na mauaji hayo.
“Huyo jamaa alikamatwa kwenye nyumba mojawapo hapo mtaani amejificha na kilichopelekea ni baada ya viatu vyake pamoja na nguo kukutwa eneo la tukio,”alieleza Lazaro.
Hatahivyo alifafanua kwamba Jambo jingine lililowatia wasiwasi ni baada ya kumkuta mtuhumiwa akiwa na majeraha ya meno sehemu mbalimbali za mwili wake kitendo kinachoashiria waliokuwa na purukushani na marehemu kabla ya mauti kumfika.
Alieleza kuwa marehemu kabla ya mauti kumfika alionekana akiwa na mtuhumiwa katika bar mojawapo mtaani hapo wakinywa pombe kabla ya kupatikana akiwa ameshafariki.
“Tukio hili limetushtua sana sisi Kama wakazi wa huu mtaa Kwa kuwa sio la kawaida lakini tumeukuta mwili wa marehemu ukiwa hauna nguo na inaonekana alibakwa kabla ya kuuwawa”alisema Lazaro.
Baadhi ya majira wanadai kwamba mtuhumiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu wakidai kwamba mtuhumiwa alikasirishwa na hatua ya marehemu kudai kutoa ujauzito wake Jambo ambalo liliibua sintofahamu.
0 Comments:
Post a Comment