MLIMA KILIMANJARO UNA UMUHIMU ZAIDI KWA JAMII

 

MLIMA Kilimanjaro una umuhimu zaidi ya inavyofikiriwa na wengi kuwa ni kwa ajili ya utalii kwani ndiyo unaopeleka maji kwenye bwawa la nyumba ya Mungu linalotumika kwa shughuli za uvuvi na kuzalisha umeme hivyo kila mmoja ana wajibu wa kulinda na kutunza mazingira ya mlima huo.



Hayo yamesemwa Desemba 9, mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaiga wakati akiongea kwenye hafla ya kuwapokea wapanda mlima 150 waliopelekea bendera ya Taifa kwenye kilele cha mlima huo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara wakiongozwa na Kanali, Martin Msumari.

Alisema kuwa maji yanayotoka kwenye mlima Kilimanjaro ni muhimu kwa maisha ya wananchi kwani ndiyo ynayotumika kwa matumizi ya nyumbani, kilimo cha umwagiliaji na kwenye bonde la Pangani.

"Watu wengi wanafikiri mlima huu uko kwa ajili ya utalii tu ila huyu mama (Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi KINAPA,Angela Nyaki) nikifika Kilimanjaro alikuja ofisini alinieleza kuwa kumbe maji ya kilimo yanatokana na mlima juu. Maji ya nyumba ya Mungu, bonde la  Pangani  yote yanatokana na mlima huu, hata  umeme wa Nyumba ya Mungu chanzo ni hapa," alisema Kigaogai nankuongeza.

....Kuanzia pale niliamua kuwa balozi wa huu mlima, na kuanzia pale nilikuwa mkali kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa, huu mlima ni kitega uchumi na ni maisha ya wananchi wa Tanzania ...

Wananchi waunge mkono jitihada za kuuhifadhi mlima huu itakuwa vibaya tukiharibu mazingira kwa kukata misitu na kufanya shuguli za kilimo ndani ya hifadhi ya mlima huu ,".

Kigaigai alisema kuwa  takwimu zinaonyesha utalii wa ndani kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro unasuasua hivyo akatoa rai kwa wananchi wa Jumiya ya Afrika Mashariki, (EAC) wajenge utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyo kwenye ukanda huo ili kukuza utalii wa ndani.



Kiongozi wa msafara huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ), Kanali, Martin Msumari alisema kuwa wapanda mlima 79 wamefanikiwa kufika kwenye kilele cha uhuru.



"Desemba 9, tuliandika historia kwa kuwa uhuru 'peak' (kilele) palisongamana watu kutoka ndani na nje ya nchi, watu 75 kufika hapo si jambo dogo," alisema Kanali Msumari.

Aidha aliuomba uongozi wa TANAPA kumtumia Mtangazaji wa Shirika la habari la Uingereza, (BBC), Salim Kikeke kama balozi wa hiari wa kuutangaza mlima huo kwani ana watu wengi wanaomfuatilia ndani na nje ya nchi aweze kuwashawishi kuja kufanya utalii kwenye mlima huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA, Jenerali Mstaafu, George Waitara, alitoa zawadi ya shilingi milioni tano kwa waongoza utalii na wabeba mizigo wa kampuni ya uwakala wa utalii ya ZARA kazi nzuri waliyofanya kuhudumia msafara huo kwa siku siku suta walizokuwa mlimani.



"Namshukuru sana mama Zara(Zainab Ansel) kwa kuweza kufanikisha zoezi hili. Kabla ya kustaafu kama mkuu wa majeshi tuliweka utaratibu wa kupanda kila mwaka nikishirikisha watu mbalimbali.  Nashukuru Jeshi wameendeleza na nilipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA nikahakikidha wanaliweka kwenye kalenda zao,"alisema Waitara na kuongeza.


.....Nilienda mpaka kituo cha Mandara ili nione watu 150 wanapandaje mlima nikajiridhisha huduma ziko vizuri, sehemu za kulala ziko za kutosha chakula kiko vizuri...


...  'Guide' (muongoza utalii) Faustini Chombo ni mzuri na timu yake alinihakikishia wengi watafika na wamefika na wagumu (wabeba mizigo) mmefanya kazi kubwa kwa kuwatambua na kuwapa soda . Nawapa shilingi milioni tano.Mmefanya kazi nzuri sana mara zote niliwaona mnatabasamu mnajitolea kuumia ili mpanda mlima asiumie,".

Alisema kuwa suala la Mtangazaji, Kikeke kutangazwa kuwa balozi wa utalii wa mlima huo ataliwasilisha kwa Waziri wa Maliasili  na Utalii, Damas Ngombaro huku akidaI anaamini atalikubali kwani anaamini mtangazaji huyo atakuwa anakuja kila mwaka na marafiki zake kwa ajili ya kupanda mlima huo .







0 Comments:

Post a Comment