KIMEI AZINDUA MRADI WA MFEREJI WA UMWAGILIAJI

 Na Gift Mathias


Moshi.

WANANCHI wa vijiji vitatu vya Rauya, Samanga na Sembeti katika kata ya Marangu Mashariki jimbo la Vunjo sasa wataweza kujikwamua kiuchumi kwa kuanzishwa shughuli za kilimo cha mbogamboga na mazao mengine baada ya mdau wa maendeleo kujenga mfereji kutoka mto Ghona wenye urefu wa zaidi ya mita 60.



Akizungumza wakati wa kuzindua mfereji huo mbunge wa Vunjo, Dkt Charles Kimei alisema mfereji huo pia utaweza kwenda hadi katika vijiji vya Matala vilivyopo katika kata ya Mwika Kusini na kuwa mradi huo licha ya kujengwa na mzawa pia una tija kwa kuchangia uchumi hususan kwa vijana.

Alisema zaidi ya milioni 17 zimetumika na kuwa wadau wengine wa kimaendeleo wanatakiwa kujitokeza kuhakikisha mfereji huo unaenda mbali zaidi na kuwa miradi mingine ya kimaendeleo inaweza kutekelezwa bila jitihada za serikali.

Katika hatua nyingine mbunge aliwataka watendaji kuachana na dhana ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wanatakiwa kuwafuata wananchi sehemu walipo ili waweze kuwatatulia shida zao

Akiwa katika kata ya Marangu Magharibi ambapo alikagua na kuridhishwa na ujenzi wa maabara  katika sekondari ya Makomu ambapo pia mfuko wa jimbo ulichangia milioni 2.5 aliwataka viongozi wa halmshauri akiwemo mhandisi kufika katika shule hiyo ili kutoa ushauri wa kitaalam tofauti na ilivyo Sasa.

"Yaani hapa tulipofikia wataalamu Kkama idara ya elimu wangekuwa wamesafika hapa au hata Mhandisi kujionea hii  kazi ambayo inafanywa na nguvu za wananchi pamoja na mfadhili lakini  Kama wametutelekeza hivii"alisema

Hali ilibadilika ghafla ambapo ilibainika katika kata hiyo hakuna wananchi wanaooatiwa huduma za kiserikali kutokana na kukosekana kwa ofisi ya kata licha ya wao wenyewe kuanzisha mchakato huo ambao nao haujazaa matunda hadi sasa.

"Ina maana hata Mtendaji ofisi huna Sasa majukumu yako unafanyaje au kila sehemu unapiga kambi?hii inawakatisha wananchi kujitolea kwa miradi ya kimaendeleo eti...

Kutokana na hali hiyo Dkt Kimei aliiomba halmashauri kuliangalia kwa upya suala hilo na kuwa kuendelea kuchelewa kukamilika kwa mbali na kukwamisha maendeleo lakini pia linarudisha nyuma jitihada za wananchi wapenda mandeleo.

Filbert Shao ni diwani wa kata hiyo na makamu mwenyekiti was halmashauri ya Moshi ambapo alisema tayari alishaomba fedha kutoka halmashauri ilu kukamilisha ujenzi huo na kuwa kunahitajika nguvu kubwa za kuihamasisha halmashauri ione umuhimu wake.

"Tunakuomba mbunge 'ukapush' (ukasukume)hili suala sababu hapa ni kama nguvu ya wananchi itakuwa zimetumiwa vibaya bila maelengo kutimia," alisema Shao.

Richard Lyimo mkazi wa kata hiyo alisema watumishi wengi wakiwemo wataalam wa kilimo hawajulikani hata sura zao kutokana na kuwa hakuna sehemu ya kuendesha majukumu yao ya kila siku.

"Hawa wangetakiwa wawe wanakuja huku ngazi za chini katika kutuhudumia lakini watakaa wapi ndio maana tulijichangisha na kufikia hapa ilipo Sasa"alisema


0 Comments:

Post a Comment