Askofu wa KKKT Daiyosisi ya Meru, Mchungaji Elias Nassari, ameongoza ibada ya misa maalum ya sherehe kumuaga (sendoff) mtoto wa mbunge Arumeru Mshariki, Dkt. John Pallangyo, Caroline anayetarajia kufunga ndoa na mbunge wa Korogwe Vijijini, Thimotheo Mzava.
Aidha aliwaasa kuwa na upendo wa Mungu ili waweze kudumu kwenye ndoa hiyo kwani wanaoweka upendo kwenye mambo ya dunia ndoa zao huishia kwenye mifarakano.
Ibada hiyo imefanyika leo, Julai 2, 2021 nyumbani kwa mbunge Pallangyo na kuhudhuriwa na watu wa karibu na familia hizo mbili ambapo baada ya ibada hiyo walishiriki vyakula na vinywaji.
Baadae hafla ya kumuaga Caroline ilifanyika kwenye ukumbi wa kituo cha mikutano ya kimataifa cha Arusha, (AICC).
"Tumelizoea neno upendo mpaka linakuwa neno la kawaida. Neno upendo si letu bali ni neno la Mungu. Upendo ni zawadi ni karama inayotoka kwa Mungu mwenyewe," amesema askofu Nassari na kuongeza .
"Na tukiishika namna ile upendo wa kweli, upendo wa Mungu ukitutawala haya mengine ya duniani yanakuwa na mashiko lakini bila hivyo haya mengine ya duniani ni ya muda sana,".
"Ndiyo sababu vijana wanaoweka mkazo kwenye upendo wa vitu vya dunia hauchukui muda wanachokana wanaachana wanafarakanana vitu kama hivyo lakini wakishika upendo wa Mungu basi maisha ni mazuri,".






0 Comments:
Post a Comment