MAPYA yaibuka kwenye kesi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya baada ya baadhi ya waandishi wa habari wanaoripoti kesi hiyo kudai kutishiwa maisha.
Kufuatia hali hiyo Chama Cha Waandishi wa habari mkoani Arusha, (APC) kimetoa tamko la kulaani vitendo hivyo vya vyenye dalili ya kuwatisha, kuwaogopesha na kuwakatisha tamaa waandoshi.
Kwenye tamko hilo lililotolewa leo Juni 22, 2021 na Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu amesema kuwa tayari mkuu wa Mkoa, John Mongela ameshapewa taarifa na ameshachukua hatua.


0 Comments:
Post a Comment