WAFANYABIASHARA jijini Arusha wameonyesha kuwa na matumaini makubwa kwa serikali ya Rais, Samia Suluhu Hassan kuwa itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli ili waendelee kujiendesha kwa ufanisi huku wakitoa ajira zaidi kwa wananchi.
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti leo Aprili 19, 2021, jijini Arusha
wakati wakitoa salamu za pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais.
Walisema kuwa, wanaamini serikali itaendeleza yale yote mazuri iliyokuwa imeanza hasa ukizingatia hotuba anazozitoa zimekuwa zikihimiza juu ya utawala bora .
Mkurugenzi wa kampuni ya Alpha Group LTD, Karim Dakik, alisema wao kama wafanyabiashara wana matumaini makubwa na uongozi wa Rais, Samia pamoja, Makamu wake Dk Philip Mpango pamoja na baraza lake la mawaziri aliloliteua.
"Nina hakika kuwa ufahamu wake mkubwa kuhusu mazingira ya biashara ya nchi yetu na changamoto zake, tutakuwa na fursa nyingi za kukabiliana na changamoto zozote zile za pamoja,".
Kampuni ya Alpha group inajihusisha na uuzaji na usambazajiwa bidhaa mbalimbali pia ni mmoja wa wakala mkubwa wa sukari mkoani hapa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha Nondo cha Bansal Steel Rolling mills, Tej Bansal mbali ya kutuma salamu za pole na pongezi kwa Rais Samia na Makamu wake, Dk Mipango naye alisema wanaamini serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wamiliki wa viwanda kama ilivyokuwa ikifanya awali.
Alimtakia Rais, Samia pamoja na wasaidizi wake mafanikio mema katika kutekeleza majukumu hayo mapya huku akiahidi kuwa wataendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali
0 Comments:
Post a Comment