VUTA NIKUVUTE UCHAGUZI TLS, WENGI WATAKA KIONGOZI ASIYE NA MAKUNDI

 JOTO la uchaguzi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) limezidi kupamba moto huku wagombea wa nafasi ya Urais wakionyesha mchuano mkali na wanachama wakiweka msimamo wao kuwa kwa sasa hawahitaji kiongozi mwanaharakati wala anayeegemea mrengo wowote kisiasa.


Wakiongea  waandishi wa habari jijini Arusha 
kwa nyakati tofauti leo April 14, 2021 wanachama hao wa TLS wamesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakiwa ni wa mfano kwani wanataka wapate kiongozi atakayejikita kusimamia misingi ya kuundwa kwa TLS.


Wagombea wa nafasi ya urais  kwenye uchaguzi huo unaotarajia kufanyika  ijumaa April 16, 2021ni pamoja na Shehzada Walli, Fransis Stolla, Albert Msando na Dk Edward Hosea.

Rais wa TLS anaemaliza muda wake ni  Dk Rugemeleza Nshala.


Mmoja wa mawakili hao, Ipiringa Panya, alisema kuwa yeye binafsi anaona kiongozi anayepswa kuchaguliwa awe ji myu mwenye malengo ya kuimarisha TLS na asiwe na makundi yanayoweza kuleta taswira tofauti na sera na malengo ya taasisi hiyo.

"Awe nu neutral na fucused , kwa sasa hivi kwa kuwa tuna mawakili wengi vijana ingependeza akipatikana kiongozi ambaye ni kijana anayeweza kujua kwa karibu mahitaji ya mawakiki walio wengi ambao ni vijana lakini ambaye anaweza kuelewa matakwa ya mawakili wakubwa," anasema Panya.


Akizungumzia madai yaliyowahi kutokewa kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiongozwa na watu waoegemea itikadi za vyama vya siasa na wanaharakati Panya anasema," Wakati umefika mawakili wachague mtu ambaye hana haya masuala ya itikadi yaani asiwe mkereketwa wa chama fulani  au mtu wa harakati,".

Alisema wanasheria chombo pekee cha kusemea mambo yao ni TLS lakini watu wa haki za binadamu yapo mashirika mengi ya kuwasemea na wasiasa kuna vyama vingi sana wanavyoweza kuvitumia kupigani agenda zao.

 "Sisi wanasheria wote nchi nzima ni wajibu wetu kulinda haki za binadamu wote na kusimamia utawala bora na wa sheria," anasisitiza Panya na kuongeza.


"Binafsi namuunga mkono Shehzada Walli kwani sera zake nimezielewa, zinagusa madlahi mapana ya wanachama wote, mawakili vijana, wakongwe na hata wakina mama ameguda ni namna gani atawasaidia,"...

"Lakini kikubwa kuliko vyote kijana huyu yeye hana makundi wala ukereketwa wa chama chochote cha siasa, yeye amelenga kuiendeleza TLS kuhakikisha wanachama wote wanapata tija na manufaa kutokana na TLS,".
 
Panya anasema anaamini Walli ataweza kuboresha mahusiano kati ya TLS na taasisi nyingine ikiwemo Serikali, mahakama hata bunge.

Wakili mwingine ambaye hakupenda jina lake lifahamike alisema kuwa TLS kwa kiasi kikubwa imeyumbishwa na watu waliokuwa wakiwachagua ambao walikuwa ni wanasiasa na wanaharakati jambo alilodai kuwa mwaka huu hawatapenda kuona likijirudia.

" TLS ni taasisi huru, tunataka ijulikane hivyo na ionekane hivyo, tunataka TLS ya kuwasemea wanasheria, tunataka TLS ya kusimamia mambo ya msingi kwa manufaa ya wananchi wote na Taifa, wanaotaka siasa wakafanye kwenye vyama vya siasa wanaotaka harakati waende kwenye asasi za kiraia za kutetea haki za binadamu," alisema wakili huyo ambaye alikataa kuweka wazi anamuunga mkono mgombea gani.

Hiki ni kipindi cha lala salama ambapo kampeni zitafungwa rasmi kesho alhamisi April 15,2021 ambapo mbali na uchaguzi wa Rais pia watachagua, Makamu wa Rais na Mweka hazina 

Tayari TLS imefanya uchaguzi kuwapata viongozi wa kanda na chama cha wanasheria vijana April 14, 2021 ambapo viongozi wote wataapishwa jumamosi April 17, mwaka huu.

0 Comments:

Post a Comment