Aliyasema hayo jana Aprili 17, 2021 wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wa jeshi la Wananchi nchini, (JWTZ) ambapo hiyo ni mara ya kwanza kwa sherehe hizo kufanyika kwenye Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.
Mwigulu alisema IAA ilitambuliwa rasmi na ACCA, Februari mwaka huu ambapo kinakuwa miongoni mwa vyuo vitatu vyenye usajili huo kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashiriki.
Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba, alisema kundi la kwanza la Shahada ya Sayansi ya Kijeshi ilifunguliwa Novemba 20, 2017 ikiwa na jumla ya maafisa wanafunzi 158 kati yao wanaume 150 na wanawake 8 .
Alisema maafisa wote ni Watanzania ambapo maafisa wanafunzi waliofikia hatua yakupata kamisheni ni 143 baada ya wengine 15 kuachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Brigedia Jenerali Mwaseba alisema kundi la 68, 2020 la mwaka mmoja, kozi ilifunguliwa Februari 25, 2020 ikiwa na maafisa wanafunzi 244, Watanzania 237 huku wa kutoka nchi rafiki wakiwa 7.
Alizitaja nchi hizo rafiki kuwa ni Falme ya Eswatini ikiwa na maafisa wanafunzi wawili na Jamhuri ya Kenya ikiwa na maafisa wanafunzi watano.
Hata hivyo, Brigedia Jenerali Mwaseba alisema maafisa wanafunzi 11 walioachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Brigedia Jenerali Mwaseba alisema kuwa maafisa wanafunzi waliofikia hatua ya kupata Kamisheni ni 226 ambapo kutoka nchi rafiki wako saba.
" Maafisa wanafunzi 17 walijiunga na wenzao baada ya kufanya mafunzo yao nje ya nchi na mchanganuo ni kama ifuatavyo, Burudi mmoja, China wawili, India wanne, Kenya watano, Moroko wawili, Ujerumani wawili na Marekani Afisa mwanafunzi mmoja," alifafanua Brigedia Jenerali, Mwaseba na kuongeza.
"Maafisa wanafunzi uliowatunuku kamisheni leo idadi yao ni 386. Wanawake 51 na wanaume 335,".
"Mchanganuo wa elimu ni kama ifuatavyo; Shahada ya Umahiri (Masters) 5, Madaktari wa binadamu na taaluma nyingine za tiba 103, Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) 1, Shahada ya kwanza ya taaluma nyinginezo nje ya tiba 271, Stashahada ya Juu 1, rubani 1 na kidato cha sita 4 ,".
IDADI YA WANACHUO IAA YAONGEZEKA ZAIDI YA ASILIMIA 100
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka, alimshukuru Rais Samia kwa nafasi waliyopewa kama chuo kwenye mahafali hayo aliyoyaita ya kihistoria.
"Tunashukuru kwa mahafali ya kwanza ya kihistoria ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa ushirikiano wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli na Chuo cha Uhasibu Arusha, hii ni heshima kubwa sana kwetu," alisema Prof Sedoyeka.
Alisema IAA kwa mwaka 2019 ilikuwa na wanafunzi 3,400 ambapo kwa idadi imeongezeka kuwa zaidi ya mara mbili kwani kwa sasa wana wanafunzi zaidi ya 7,000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 100.
Prof Sedoyeka amesema kuwa huo hicho kina kampasi tatu za Arusha, Babati na Dar es Salaam.
0 Comments:
Post a Comment