MUUGUZI AJINYONGA KISA MADENI


MUUGUZI wa hospitali ya wilaya ya Arumeru, David Mtaita, (30) amejinyonga kwa kutumia kamba hadi kufa baada ya kuzidiwa na madeni.



Taarifa ya kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo aliyoisambaza kwa waandishi wa habari jana Aprili 28, 2021 imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Aprili 24, mwaka huu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa tukio hilo limetokea maeneo ya Sing'isi tarafa ya akheri wilayani Arumeru majora ya saa 12.40 jioni.

"Baada ya kufanya uchunguzi wa kina Jeshi la Polisi lilibaini kuwa marehemu alikuwa na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni mengi yanayomkabili kitendo ambacho kilimpelekea kuchukua hatua hiyo ya kujinyonga," inaeleza sehemu ya taarifa ya kamanda, Masejo na kuongeza.

"Pia uchunguzi huu ilibainika kwamba, kabla ya marehemu kujinyonga alijidunga sindano ya kupunguza maumivu aina ya LIGNOCAINE kisha kujinig’iniza kwa kamba ya urembo wa mapazia iliyofungwa juu ya ubao wa ceiling board kitendo kilichopelekea kupoteza maisha,".


"Nitoe wito kwa wananchi kuto jichukulia maamuzi mabaya kama hayo na 

badala yake mnapaswa kwenda katika maeneo maalum kupata ushauri 

ambao unaweza kuwa suluhu ya matatizo yao kuliko kuchukua uamuzi wa 

kujitoa uhai,".

1 comment:

  1. Hii ni hasara hata kwa wanao mdai tujifunze kudai kwa staha maana ukinikera najinyonga ili nikukomeshe..

    ReplyDelete